Kwanini wastaafu wa Tanzania hawawekezi kwenye sekta ya viwanda?

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
Wastaafu wa Tanzania wanaoonekana wana akili na maono wengi wanawekeza kwenye nyumba za kupangisha, kujenga fremu za biashara na kuzipamgisha, wengine wananunua bodaboda 10-20 kwa mkupuo na kusubiri hesabu ingawa baada ya muda wanapigwa na kitu kizito kichwani.
Wengine wanawekeza kwenye kilimo cha mpunga, miti ya mbao na biashara zingine.
Shughuli nyingi za kiuchumi zinazofanywa na wastaafu hazina tija kubwa kwenye uchumi wa nchi.
Kuna viwanda vya chuma , kuna aina nyingi za mazao yanalimwa Tanzania. Ni wakati sasa serikali iwasapoti wastaafu wapate kuanzisha viwanda vidogo na vya kati kwa kushare .
Waitwe wataalamu India na China wastaafu wafundishwe kuzalisha angalau bush za pikipiki na magari. Soko lipo.
Wastaafu wafundishwe kusindika mazao ili wasafirishe.
Pamba zipo za kutosha viwanda vidogo vya nguo pia ni fursa .
Nchi imejaa mafremu mpaka kinyaa.
 
, ughuli nyingi za kiuchumi zinazofanywa na wastaafu hazina tija kubwa kwenye uchumi wa nchi.

Leo umeamka nasi. Subiri nawe ustaafu ulipwe million 20 na uanzishe kiwanda
 
unajua wastafu wanalipwa kiasi gani au unajiropokea vile tu umeshiba
jiheshimu rafiki
tena waonee huruma wastaf
kwamba hujasikia malalamiko ya kikotoo
 
Umesema wengi wanaonekana wana akili,
Hayo ya kuwekeza kwenye viwanda kwa mfano, ni hela ndefu sana labda vya cherehani
Biashara inataka ushirika wa watu kadhaa
Sisi hatuna tabia ya kuwa partnership kwenye sekta za viwanda

Duniani na mataifa mengi wanafanya hivi ila sisi uaminifu ni mdogo sana

Hata vijana mnaweza achana na wazee maana wao wameamua hivyo
Kiwanda cha Textiles majengo na eka zote wamenunua NHC na watu wanapiga kelele ooh bei ndogo sana 3b na kwanini wajenge majumba
Ni kwa sababu mji umekuwa viwanda vipelekwe nje ya mji ila hata huko nje ya mji hakuna kitu

Haya watu 20 kila mmoja aweke 100m tufanye jambo hapa kiukweli
 
Wapo niliona makala moja wameungana wana kiwanda kidogo cha kukoboa,kusaga na kufungasha nafaka na wengine wanakamua mafuta ya alizeti.
Tatizo hawafiki mpaka kuitwa billionaires hii ndio shida yetu
Yaani wanaridhika mapema au hawajui kupanda ngazi

Dangote alianza na biashara kama hiyo ya kusaga na kufungasha na leo ni tajiri mkubwa Africa
 
Pesa ya kustaafu ikutane na biashara ambayo tayari ilishasimama, la sivyo utawaua kwa presha wazee wetu

Wengi hawana uzoefu na biashara na hawajawahi kufanya biashara, acha wawekeze humohumo ambapo hakutawaumiza vichwa na presha
 
Wastaafu wa Tanzania wanaoonekana wana akili na maono wengi wanawekeza kwenye nyumba za kupangisha, kujenga fremu za biashara na kuzipamgisha, wengine wananunua bodaboda 10-20 kwa mkupuo na kusubiri hesabu ingawa baada ya muda wanapigwa na kitu kizito kichwani.
Wengine wanawekeza kwenye kilimo cha mpunga, miti ya mbao na biashara zingine.
Shughuli nyingi za kiuchumi zinazofanywa na wastaafu hazina tija kubwa kwenye uchumi wa nchi.
Kuna viwanda vya chuma , kuna aina nyingi za mazao yanalimwa Tanzania. Ni wakati sasa serikali iwasapoti wastaafu wapate kuanzisha viwanda vidogo na vya kati kwa kushare .
Waitwe wataalamu India na China wastaafu wafundishwe kuzalisha angalau bush za pikipiki na magari. Soko lipo.
Wastaafu wafundishwe kusindika mazao ili wasafirishe.
Pamba zipo za kutosha viwanda vidogo vya nguo pia ni fursa .
Nchi imejaa mafremu mpaka kinyaa.
Kwanza hao wanaojenga fremu wamejitahidi sana japo wengine wanaojenga fremu wanazijenga sehemu ambazo ni kando kabisa na makazi ya watu kiasi kwamba mtu hapati genye ya kupangisha hapo tu ndo wanafeli ktk hilo.
 
Kwa nini wajenge Viwanda Wakati Hawana maarifa na Ujuzi wa Viwanda??
Kiwanda linahitaji mtaji (Pesa,Ardhi,Ujuzi,Maarifa, Taarifa NK).Ungesema wastage wawekewe biashara wanazouza.Mfano Mwalimu ajenge na Kuendesha Shule,Mtaalam wa Afya ajikite Huduma za Afya, Mhasibu afanye uhasibu kama mtaalam mashauri.Unakijua kiwanda?Unajua vibali vyake?Unajua bidhaa zinazoingia bila Kodi toka Nje?Unajua ubovu wa miundombinu nchini?Unajua Wizi na udokozi wa Wafanyakazi?Unajua malighafi feki?Unajua danadana za TRA na mabenki?
Unataka watu wage Kwa Kuendesha kiwanda?Nimeshafanya Kazi kwene kiwanda,najua lash zake.Kama huna roho ngumu hutoboi.Maeneo Salama Kwa wastage ni bonds za Serikali,UTT,Nyumba za kupangisha.Usisahau Kikokotoo,hivyo Pesa inalipwa ndogo Sana.Nina ushuhuda wa Jamaa yangu alistafu na kuanzisha Kiwanda kidogo cha Kukamua Mafuta ya mbegu.Ni Mhandisi,ila Miaka 3 ilikuwa mingi ameuza Mashine zote na kurejea kwenye Kupangisha Nyumba.TRa walimpiga kitu kizito pressure ikapanda.
 
Ukisikia viwanda vidogo, humo ndani hakuna utendaji wa ki viwanda.

Ukienda huko saba saba waonesha mashine na bidhaa za viwanda ni sekta binafsi. Yaani mtu anaambiwa njoo upange bidhaa yako hapa eneo la viwanda.

Hiyo miaka yangu mingi niliyotumika huko viwanda hata kutengeneza batiki au mshumaa sijui. nimekuja kulipa mmama huku mtaani ndiyo akanifundisha.

Pengine sasa viwanda I mean SIDO mjiumbe upya.
 
Mkuu kiwanda sio lelemama acha wawekeze kwenye majumba Mimi hata mstaafu simshauri kufanya biashara za kukimbizana kwanza umri ushamtupa mkono just imagine kipindi yeye ameanza kuajiliwa wenzake wakaingia kwenye biashara sasa Leo amestaafu na yeye ndio aingie kwenye biashara atakufa mapema sana by da way umri wako mleta mada??? tafadhali
 
Serikali yenye mapesa na wafadhili wa kutosha hivyo viwanda vya kutengeneza vifaa vya pikipiki viko wapi? mpaka utolee macho pensheni za wastaafu? unafahamu pensheni ya wabunge na mawaziri? mbona hatuoni wakifungua hivyo viwanda wakat wao wana access ya kupata hata wahisani? kweli mwl na pensheni ya miln 50 ndo aanzishe kiwanda?
 
Back
Top Bottom