Kwanini Watanzania hatutaki kutangaza na kujivunia vya kwetu, ni ushamba?

Kwanini Watanzania hatutaki kutangaza na kujivunia vya kwetu, ni ushamba?

Wakili wa shetani

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2022
Posts
1,726
Reaction score
3,391
Kwanza niwapongeze Tamisemi kwa kuja na hii huduma ya kupata leseni mtandaoni. Haya ni mapinduzi makubwa sana kwenye uwezeshaji wa biashara. Lakini nina kero moja amabyo kijuu juu inaweza kuonekana ndogo lakini ni kubwa sana. Kwa nini mmetumia jina na nembo ya ndege tausi.

Nilidhani TAUSI ni kifupi cha jina fulani lakini sijaona. Tausi ni ndege ambao asili yao ni Asia. Watu wengi watapita mle ndani, kwa nini tuwatangaze ndege wa bara lingine, sisi hatuna ndege wetu wazuri wa kutumia? Mbona tuna kanga na secretary birds na ni ndege wazuri.

1692859420879.png
 
Ndege/Wanyama wengi wanakuwa na aina tofauti, Kuna Tausi wa Asia na Africa, Tembo wa Asia na Africa, Simba wa Asia na Africa etc.

Tanzania pia kuna Tausi, ila wapo wengi zaidi Congo basin, ukiangalia Tanapa utaona ni katika wanyama pori tulionao.

Ukitoa Origin ya Yake huyo Ndege Artistic point of view Tausi aliyewekwa ana rangi ya Kijani, Njano, Nyeusi na Blue, Rangi za bendera ya taifa.
 
Wale wa Congo ni tofauti sana na hawa wa kawaida. Na Tanazania hakuna tausi wa asili. Hapo kwenye rangi ya taifa nimekupata kiasi.
 
Back
Top Bottom