Johnny Sack
JF-Expert Member
- Jan 21, 2017
- 8,984
- 19,288
Ebana kama mnavyojua timu yetu ya wanawake chini ya miaka 17 Serengeti Girls imefika robo fainali Kombe la Dunia baada ya kuwachapa vigogo wa soka Ufaransa na Canada.
Lakini Watanzania hawaonyeshi hata kushtuka, hakuna shamrashamra yoyote ya maana. Habari ya michezo inayovuma ni Simba na Yanga kwenye michuano ya Club Bingwa Afrika, ambayo ni michezo midogo sana ukilinganisha na Kombe la Dunia.
Hata wachambuzi wetu wa michezo hawaichambui kwa mzuka kivile, kama wanajilazimisha vile. Nasikiliza Sports HQ hapa Tunu Hassan anamuliza Maestro maoni yake kuhusu hili ila jamaa anajibu kwa kifupi kama vile hataki.
Ni kuwa watu hawana imani na hii timu kuwa imeshinda kihalali bila magumashi ya kufoji umri au hawana uzalendo? Maana Tanzania haijawahi kufika hatua hii kwenye hatua ya Dunia.