Kwanini Watanzania hawana mzuka na Serengeti Girls kufika robo fainali Kombe la Dunia la Wanawake chini ya miaka 17?

Johnny Sack

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2017
Posts
8,984
Reaction score
19,288
Ebana kama mnavyojua timu yetu ya wanawake chini ya miaka 17 Serengeti Girls imefika robo fainali Kombe la Dunia baada ya kuwachapa vigogo wa soka Ufaransa na Canada.

Lakini Watanzania hawaonyeshi hata kushtuka, hakuna shamrashamra yoyote ya maana. Habari ya michezo inayovuma ni Simba na Yanga kwenye michuano ya Club Bingwa Afrika, ambayo ni michezo midogo sana ukilinganisha na Kombe la Dunia.

Hata wachambuzi wetu wa michezo hawaichambui kwa mzuka kivile, kama wanajilazimisha vile. Nasikiliza Sports HQ hapa Tunu Hassan anamuliza Maestro maoni yake kuhusu hili ila jamaa anajibu kwa kifupi kama vile hataki.

Ni kuwa watu hawana imani na hii timu kuwa imeshinda kihalali bila magumashi ya kufoji umri au hawana uzalendo? Maana Tanzania haijawahi kufika hatua hii kwenye hatua ya Dunia.
 
Hii timu wakiingiza tu mkono wale wanasiasa nuksi wa kijani inatolewa bora ibaki hivyo hivyo wapige mbungi kimya kimya.
 
Wanawake wasitake mba mba mba nyiiingi za kisiasa mambo yatakwemba kombo. Wapigane kimya kimya waje na kombe ndio tufurahie wote.
 
Kwani yaliyoikuta TWIGA STARS huyajui? Taifa stars kusifiwa na kupelekwa bungeni na kupewa viwanja kilichowakuta hukijui? Hata YANGA SC wakitaka kufanikiwa wanapaswa kwenda kimya kimya kwani shangwe , kelele na sifa hazijawahi kumwacha mtu anayevaa kijani & njano salama.
 
tukiwa na vibe nao wakavuma,ghafla utasikia Shaka Hamdu Shaka ndo mlezi wa timu.ni bora iyo timu tuiache isipate kiki isije kua CCM wakaitumia kujinufaisha.
Hahaha hahaha haaaaaaa hahahaha haaaaaaa haaaaaaaaaaa.
 
Tunawaaminia sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…