Kwanini Watanzania tusianze massive constructions of apartments nchi nzima?

Muongo huyo China 1980 haikua sawa na Tanzania kiuchumi. China ilikua top 10 duniani kwa uchumi mkubwa
Kwanza nani kasema China ilikuwa sawa na Tanzania kiuchumi.
Mwenzako kaongelea per capita income kasema pato la Mtanzania kwa mwaka ni 2.5 million Tsh, yani unafananisha mapato vs population. China leo hii ni ya pili kwa uchumi mkubwa duniani lakini inazidiwa per capita income na nchi nyingi duniani.
Miaka ya 1980s China ilikuwa na per capita income ya $195, wananchi wengi walikuwa hawajiwezi

Mfano rahisi, unajua kuwa India ipo top 5 nchi zenye uchumi mkubwa duniani lakini wananchi wake wengi ni masikini wa kutupwa?

Vitu vingine kama vipo nje ya uwezo wako sio lazima uchangie. Huelewi vitu tunavyoongea halafu unatumia lugha kali ni kama uko na anger issues ndio maana nilikuwa najaribu kuignore comment zako
 
Nimekuuliza hapo uchumi unapimwa kwa per capita tu? Wanaojenga hiyo miradi ni serikali, niambie kwa uchumi huu wa nusu kulipa deni nusu kulipa mishahara wapi watapata pesa za kujenga kama China?
 
Uchumi unapimwa kaa per capita tu?
China ya 1980 ambayo ilikua na gdp ya $300 billion ukafananishe na Tanzania ambayo hata sasa haijafika hata $100billion
Kuna vitu unachanganya. China ilikuwa na $300B economy huo mwaka 1980 lakini at the same time ilikuwa na wananchi milioni 900+ meaning ilikuwa na watu wengi sana wa kuwahudumia lakini bado walihangaika kusaidi population yao mdogomdogo hadi leo wamefanikiwa kugusa population kubwa

Tanzania ina $95B economy, na wananchi takribani 65M+ kwa hiyo uchumi wa Tanzania unatosha kabisa kuanza project za makazi sasahivi kama China ilivyoanza miaka ya 1980 kwa 300B huku wana watu milioni 900+ wa kuwahudumia
 
Tuko wengi mkuu wenye mawazo kama Yako.
Juzi kati Kuna sehemu nilikuwa nafanya kazi, mtoto mdogo kabisa (Yuko darasa la nne au Tano ) akamuuliza baba yake "Baba Kila sehemu mnajenga nyumba, kwanini usijenge nyumba kuuubwa Ili watu wote waje wakae humo?
 
Nimekuuliza hapo uchumi unapimwa kwa per capita tu? Wanaojenga hiyo miradi ni serikali, niambie kwa uchumi huu wa nusu kulipa deni nusu kulipa mishahara wapi watapata pesa za kujenga kama China?
In short unauliza Tanzania yenye $95B na wananchi 65M+ itapata wapi pesa za kujenga kama China yenye $300B ilivyowajengea wananchi milioni 900+???

Huoni kama Tanzania ndio ipo kwenye better position ya kujengea wananchi sasa kuliko China ilivyokuwa mwaka 1980? Fanya comparison ya hizo figures hapo juu (95B for 65M+ vs 300B for 900M+)
Kwa China tuna vingi vya kujifunza, sio tu apartments. Wakati wanajenga apartments walikuwa wanajenga viwanda pia na sisi tupite humo, kwani si Mwalimu Nyerere dam ilijengwa ili tuwe na umeme wa viwanda. Tuongeze uzalishaji sasa huku tunajenga makazi bora. Tuna nafasi kubwa sana ya kuanza kuwa na viwanda vya nguo, madaftari, TVs, subwoofers, rice cooker, vyombo vya nyumbani, water heaters, mafriji, majiko ya gesi, charger za simu, flashi, nyaya za umeme nk. Kuna vitu vingi sana tunaagiza kutoka nje wakati vinaweza kuzalishwa hapahapa Tanzania. Huo ni mfano tu, sio viwanda pekee sasahivi naona tunaboresha elimu ya ufundi, nk. Tanzania ina potential sehemu nyingi tu hata kilimo, usafirishaji, uchimbaji na uuzaji wa madini. Njia walizopitia China tunaweza kuzipitia.
Kama nchi haina hela basi iongeze uzalishaji at the same time iwe inajenga makazi mdogo mdogo.
Hivi unajua kuwa Kenya in recent years wameshaanza ujenzi wa apartments nchi nzima kwa ajili ya wananchi wa chini na kati? What makes you think that Tanzania can't?
 
Hakika mkuu, ujenzi wa makazi ya watu wengi kwa eneo dogo ndio unafaa kwa dunia ya sasa. Dogo alikuwa sahihi na ni great thinker, kwa sasa miji yetu ipo kwenye rapid urbanisation and we have to do something now maana tukiendelea hivi hadi miaka 30 ijayo hali itakuwa mbaya
Ni useless kufosi watu wajenge wenyewe halafu outcome inakuwa hivi
 
Unajaribu kufananisha Mchina na Mtanzania kweli ?
Hata IQ level tu hawapo sawa
 
Mkuu umesoma uchumi ?
 
Nchi haina Rais ina kiazi, unategemea nini?
 
Urban spraw kwenye well organized plots sio shida na inaweza kuhimilika kuliko squatters.

Saizi ukianzia Uyole Hadi Songwe ni squatters along the main road.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…