Kwanini Watanzania wengi hawajui/hawafanyi Biashara za Exportation kwenye mazao ya Kilimo?

Lasway.Jr

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2015
Posts
233
Reaction score
413
Hebu kila mmoja atupe uzoefu wake kwenye biashara za exportation

Au useme ni sababu gani zinakufanya ushindwe kufanya exportation

Mimi nitaeleza kidogo:

Leo nimeona tujadili kidogo ni kwanini sisi watanzania tunalima na tuna Ardhi nzr sana lakini hatufanyi Biashara kubwa kwenye kilimo yaani exportation , badala yake wakenya ndio wanatupiga Mzinga na kumiliki Biashara hizi Je? Tulichelewa WAP? Au ni nini ambacho hatuji?

Nitaeleza kwa namna ambavyo nimefanya utafiti wangu na kugundua mambo kadhaaa:

Kwanza kabisa, watanzania wengi sio wakulima (we a not Farmers rather we are peasants) nikiwa na maanisha kuwa hakuna mtanzania au hata kama wapo ni wachache wanaoweza kulima kuanzia hekari 50+, 100+, 250+ kwa pamoja na kuzalisha bidhaa za kilimo , kwa hyo ni ngumu kufanya Biashara za exportation kwa sababu hatuna vigezo hivyo

Pili, tulio wengi tumekuwa nyuma sana kwenye matumizi ya teknolojia pamoja na matumizi ya utaalamu kwenye kilimo vitu vya msingi kama soil test, water test, farm planning, post harvesting handling, pack house, ware house management na vingine vingi watanzania wengi hatuvijui na hatuna elimu yake , nimeeleza baadhi ya hivi vitu kwa sababu ili uweze kufanya exportation kwa baadhi ya mazao lazima uwe na certificate za taasisi ya kimataifa ya GAP sasa hawa wana vigezo na masharti yao ambayo yanaendana na vitu nilivyotaja hapo juu

Nilipokuwa naendelea kufanya utafiti kuona nani ametuloga niligundua kuwa Tanzania hasa wakulima hatuna taarifa sahihi kwenye masoko ya bidhaa za kilimo na pia tumewekuwa watu wa njaa sana na kuuza mazao Yetu Mara tuu tunapovuna kwa kuona fursa ya sisi kuwa wavivu ndio maana wahindi na waarabu ndio nakumbana nao huko masokoni kwenye Biashara kubwa za exportation na wanapata faida kubwa sana sio sana tuu faida kubwa mno (mfano mzr ni kwenye korosho) miaka yote hawa jamaa walikuwa wanapata faida kubwa kiasi gani ? Kwa sababu wakulima wananunua korosho kwa shilingi 500-1500 kwa kilo na sasa korosho hyo hyo inauza 4000 kwa kilo na wananunua just imaging

Kwa ndugu zetu wakenya matajiri wengi ni wakulima lakini sio ajabu sana kwa Wakenya kutupiga vikumbo kwenye exportation kwa sababu settlers walioanza Kilimo Kenya miaka ya 1885+ mpaka Leo wapo so not bad because their trade back home ndio maana Kenyan wanaexport sana UK, lakini soko lao liko vizuri kwa sababu wana certificate za mashamba ambazo hutumika kufanya exportation iwe rahisi hasa kwenye mazao ya matunda na mboga mboga kwa hiyo wanachofanya wanakuja Tanzania wananunua mazao yetu then wanatumia certificate na label zao wanauza Ulaya

Nyingine ni kwamba Tanzania tuna viongozi wengi sana ambao sio wafanyabiasha na wengi ni maskini ndio maana wakienda ulaya wanarudi na laptop na camera na wanasahau kurudi na connection za Biashara, hata wasomi wengi wanaokwenda kusoma wanarudi bila connection yoyote kitu ambacho wakenya wakienda wanarudi na akili ya Biashara kubwa, nafurahia sasa vijana wetu walioenda kusoma China wa nafanya Biashara sasa na jambo jema

Ukitaka kuanza Biashara ya exportation kwa Tanzania anza na dry food na sio mboga mboga kwa sababu hizi zinahitaji regulations nyingi sana , but grain ziko vizuri sana, na pia ukitaka Biashara ya exportation ikae vizuri anza na zile nchi ndogo Scandinavian countries, Asian, etc Ulaya kuna milolongo mingi, mimi nimeanza kidogo na nitaleta mrejesho hapa mambo yakikaa vizuri.

Hebu kila mmoja atupe uzoefu wake kwenye Biashara za exportation

Au useme ni sababu gani zinakufanya ushindwe kufanya exportation

===

Baadhi ya michango...



 
Na kingine ni marufuku za serikali kuuza mazao nje ya nchi. Wakulima hasa wadogo hawana taarifa za soko la nje, lakini wanunuzi wengi wanajua, ila katazo la serikali ni kikwazo.
 
Uzi mzuri sana lakini sitoshangaa ukiwa na wachangiaji wachache.

Binafsi napenda sana Biashara za Exportation kiukweli zinafaida sana na hizi fursa wanafaidi watu wachache wanaojua ABC za kufanya exportation, Kuna mtandao mmoja jina lake limenitoka kidogo huwa nasikia ni wazuri sana kwa kuunganisha international buyer & seller.

Mkuu vipi wewe umeanza jaribu na zao gani??
 
Taarifa sahihi za Mbegu na masoko bado ni tatizo kubwa kwa wakulima wengi nchini, Gharama zinazochajiwa na wakaguzi wa kilimo na Mbegu mashambani nalo ni tatizo ndomana wakulima tunatumia local ways.

Ila kwa hii inshu ya exportation umenigusa sana, Napenda tu kujua kwa hapa nchini ni taasisi zp ambazo znachek ubora wa mazao na ku'issue vibali, na taasisi za nje ambazo unaweza ku-link nao ili kuwa na uhakika wa soko?
 
Asilimia kubwa ya wakulima ni wadogo kwa kiwango (peasants) na hivyo ni vigumu kwao kuwa na ufahamu wa mambo kama haya.. Wale wachache wanaoweza kujua mambo haya wamejikita zaidi kwenye upagazi (a.k.a. ajira) maofisini.

Kama ulivyosema, kwa Kenya viongozi wengi ni wafanyabiashara, kwa hiyo inakuwa rahisi kuwa na sera/sheria ambazo ni rafiki kwa biashara.

Nimewahi ku export kidogo seafood. Nilipeleka mara kadhaa kaa hai Singapore. Changamoto niliyokutana nayo ni vifo vya kaa, maana mzigo ukifika kule wanahesabu na kulipia walio hai tu. Hapa inawezekana mnunuzi asiwe mkweli juu ya kiwango cha vifo maana mzigo unatuma kwa ndege.. Lakini pia kwa hapa Tz usipokuwa makini unauziwa kaa ambao tayari wamechoka kutokana na kukaa siku nyingi tangu wavuliwe.

Kuhusu samaki frozen na fresh, changamoto ni kuwa, Fisheries (wizara ya uvuvi) wanataka uwe na kiwanda kilichoidhinishwa kwa ajili ya kuandaa mzigo. Kama huna kiwanda, uingie mkataba na kiwanda then ndo wizara watakuruhusu. Ukienda viwandani, vyote ni vya wahindi, na hawa wahindi hawakubali jambo hilo ili waendelee kufanya biashara wao tu
 
Naona tunaendelea na kasumba ya kulaumiana wabongo. Hakuna mkulima asiyependa kuuza nje ya nchi mazao yake maana huko ndio kuna faida kubwa kuliko soko la ndani ambalo halina uhakika wa bei. Leo korosho wanacheka lkn uhakika wa bei kuendelea kuwa nzuri bado haupo wakati huo mbaazi imeachwa shamba ng'ombe wanaila

Anyways point yangu ni kwamba, unaposema kuwa mkulima wa Tanzania anatakiwa abadilike aanze kuuza mazao nje tujiulize hilo soko la nje lipo wapi? Tatizo ni hizo connection za masoko ya nje. Wahindi wameshikilia hii biashara sababu wana connection ya wahindi wenzao huko india na Asia. Mimi mmatumbi napataje hiyo connection ya wateja wanao hitaji zao langu nje ya nchi?

Cha kufanya watu Kama mwenye thread hii ambao mmefanya research msiwe wachoyo, leteni taarifa za masoko ya nje muone kama watu hawaja changamkia fursa. Ukituambia unafanyia kazi utaleta mrejesho ndio hatukuoni Tena au hata tukija kukusikia huo mrejesho hautakuwa na taarifa za kina za hao wateja wa nje.

Kifupi selfishness/ubinafsi ndio vinatutia umasikini. Humu ndani kuna nyuzi nyingi tu za exportation na kwenye hizo nyuzi kuna watu ambao wana uzoefu na connection lakini hakuna hata mmoja aliyetoa contacts au maelezo yakinifu ya hizo connection wanaishia kujitapa tu. Hawa viongozi Wa serikali waacheni hata mkiwapa lawama wao hawana habari hivyo tusaidiane sisi wenyewe
 
Ila nafikiri wakulima wetu ifike mahali wabadilike kama unahitaji mafanikio fulani halafu ni mzito kujielimisha kuhusu njia sahihi za kuyafikia bási itakuwa shida.

Wakenya ni more agressive sana kwenye masuala kama haya miaka ya nyuma hapo kuna mkenya alikuwa anakuja kulangua vitunguu Singida na Asali Tabora; huyu jamaa alikuwa anafanya package na branding halafu ana export Asia sasa jifikirie ni faida gani alikuwa anatengeneza?
 
Kuna mazao yenye vibali maalumu kama kahawa, korosho, pamba, etc , kuna mazao mengine hayana vibali maalumu rather utatakiwa uende wizarani pale watakupa maelekezo
 
Sijasikia habari ya vyama vya ushirika nahisi vina jukumu pande hizi!Je vimeshindwa au ni nini msingi wa vyama vya ushirika!.Kingine pia mitaji hao wakulima wakenya wanakopesheka vipi hawa wakwetu siamini kwamba ukosefu wa elimu wala connection ndo changamoto kubwa kwenye kilimo chetu la hasha!
 
sad experience
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…