Kwanini Watanzania wengi hawajui/hawafanyi Biashara za Exportation kwenye mazao ya Kilimo?

Habari za asubuhi naomba na mimi niongezee jambo hapo kwenye usafirishaji wa mazao. Miezi miwili nyumba alikuja rafiki yangu akanipa mchongo kuwa kwa sasa majirani zetu wa Rwanda wana njaa kupita kiasi.
Basi tukaenda boarer ya Rwanda tukaulizia nini wanahtaji hakutupata ushirikiano mzuri kabisaa
jamaa ikabidi azame ndani Kigali kabisaa huko akaja na fursa kede kede kweli njaa ipo Rwanda na wanahtaji sana msosi.
Basi tukajipanga kutafta vibali jamani asikwambie mtu vibali vya kusafirisha mazaoi nje (hata hapo Rwanda) ni vingi utazani daftari la tution.
Sasa tukaamua kuwa bora tu base na boarder ya Rwanda na wao wakatupa conditions zao baada ya hapo tukatafta gari maeneo ya kahama hapo tukachukuwa mzigo tukazama Kigali jamani mzigo uliisha ndani ya saa moja tu na hapo tuliuza kwa gharama ya juu sana.
tukarudia mara nne hadi sasa tunategemea kurudia mara ya tano sasa.


Nilichojifunza katika biashara hii jamani. Ku export mazao kunahtaji uwe umejipanga kabisa na sio kukurupuka kama hapa wanasema sehemu fulani kuna soko la nyanya hapana soko lipo ila lina vigezo vyake balaa. Elewa vigezo vyote vya soko lako ndio uingie mfano sisi tulisikia Rwanda wanahitaji mihogo saana, na hata askari wa boda walisema mihogo inahtajika sana. Sasa tungekurupuka kupeleka mihogo Rwanda bila kuingia Kigali na kujua mihogo hiyo inahtajika katika hali gani mzee si tungelia jamani.

kingine nchi yetu siasa ni nyingi mnoo n uongo uongo ni mwingi sana, mfano hapa bongo wakulima wa mihogo wameaminishwa kuwa soko liko China ooh ni zuri nk wakat hapo Kigali mihogo ukiiprocess wanavyohtaji wao ni kama dhahabu. Hapo kigali viazi ni dili sana sana.
Tuweni serious na maisha jamani hakuna mafanikio ya bila kujitoa na kutoa jasho
 
Mmekalia chama kimoja toka Dunia imeubwa unadhani kitabadilika nini ?

Katiba ni hiyo hiyo toka babu hadi kitukuu anaitumia haya wajameni
 
Elimu yetu duni+ Siasa zetu taabani
 
mambo ni moto napenda kilimo sana sema sinapesa yakuanzia
 
Wachangiaji wengi kwenye hii mada nahisi wakati Tanganyika inapata uhuru walikuwa hawajazaliwa.
Tatizo kubwa la Tanganyika/Tanzania katika kukuza uchumi ni mabadiliko ya mara kwa mara ya Political economy yaliyokuwa yanafanywa.
....Kabla ya Uhuru uchumi wetu ulikuwa wa Kipebari/kabaila.
.... Baada ya Uhuru kulitokea mabadiliko makubwa ya uchumi kwa kufuata uchumi wa Kijamaa na kubinafsisha mali za watu binafsi na kuzifanya za umma.
....Baada ya ujamaa kushindwa tukarudi tena kwenye ubebari /ukabaila uchwara ambao bado hauko wazi katika kumiliki mashamba na viwanda kwa uhuru.
Mfano mzuri kwa Inchi zilizofanya makosa kama ya Tanganyika/Tanzania ni Zimbabwe.
Kenya hawakubadili mfumo wa uchumi wa Inchi toka wapate uhuru hadi leo.
Tunasema kila siku Inchi ambayo haina consistence katika Political economy kamwe haiwezi kuendelea kiuchumi.
Katika hili lazima tutofautishe swala la Education na Knowledge.
Education tunaipata darasani na knowledge (ujuzi) tunaupata kwa kufanya kazi.
Watanzania wengi wanafikiri wakisoma sana darasani basi wamekamilika. Ni heri ufanye kazi na mtu mwenye ujuzi (knowledge) lakini hana elimu kubwa kuliko kufanya kazi na mtu mwenye elimu kubwa lakini asiye na ujuzi.
Tanzania bado ni Inchi bora nadhani Duniani katika mazingira rafiki ya kujenga viwanda, kulima, kuchimba madini, bandari za kutosha, maziwa ya kutosha, mali asili kama wanyama na mbuga za wanyama, mito ya kutosha na kubwa kuliko yote AMANI YA INCHI.
Kenya katika haya yote wako nyuma mno na future yao baadaye wataitegemea Tanzania.
 
Katika sekta ambayo ni muhimu na ambayo haijatiliwa mkazo na tawala ni kilimo. Ukweli ni kwamba Gold ya kweli ya Tanzania ipo mashambani hii ingetoa forex nyingi sana na kuchangia ukuaji uchumi. Hivi kwa mfano wizara ya kilimo ingekuwa na kitengo kidogo tu kinachoshughulikia kutafuta masoko ya nje na kurasimisha taratibu za kupata vibali japo kutoa tu elimu kwa wakulima ingekuwa ni msaada mkubwa sana mfano kama ilivyo utalii kuna kitengo cha kutafuta masoko nje ya nchi, vivyo hivvyo iwe kwenye kilimo. Karne hii nchi ikiendelea kulima kwa ajili ya kujitoshelza (subsistence) haitoweza kusonga kamwe. Mambo haya yabahitaji kufuatiliwa kitaasisi maana mengine huusisha pia diplomasia za kimataifa. Kilimo bado ndio mtoa ajira mkubwa nchini bila kuweka mipango mathubuti itachukua muda sana kupata matokeo sahihi.

Mbadala basi hata kwenye nchi nyingine za kiafrika tujue nini kinauzika pale. Watanzania ifike mahali tuanze kusafiri kutafuta fursa sio kila mara kwenda china tu kuimport na sisi tutafute masoko nje zaidi pia kutumia fursa za internet haswa waliopo katika sekta kilimo.
 
ila pia viongozi wetu ndio tatizo kubwa zaid. hakuna mtu siriaz wa kulisaidia hili taifa zaid ya matumbo yao.kuna mfano mawaziri huwezi jua nini anafanya na tija yake. mfano viwanda, mifugo nk serikali ingewekeza ktk kuwezesha yaan kutoa elimu ya exportation. lkn waowao tena ndio hawataki tulime tuuze nje na ukiwstaka wao wanunue hawana hela.
 
Kat
Nakuunga mkono asilimia zote.hapa tuilaumu CCM na serikali.unajua serikali haioni kua kilimo ni biashara kama biashara nyingine tu.Ndio maana wakawafundisha watu kua eti mahindi au ngano si mazao ya biashara! Ukiyalima mazao ya aina hio ya nafaka unaambiwa usiuze nje au unapangiwa bei..sasa huyo mkulima ataendeleza vipi kilimo chake? Serikali itoe hofu ya kuogopa njaa.ijenge silos za kisasa wanunue nafaka wazihifadhi.wakulima wapeni uhuru wakuuza popote na mda wowote.kuhusu masoko tuna watz wengi wapo nje tayar wanauwezo huo.hata hapa ktk nchi za jirani kama zimbabwe, kongo au botswana tunaweza anzia
 
Hapo umenigusa penyewe cheef, yani kiukweli najiskia uchungu sana kule kijjn kwetu tulivokuwa na ardhi nzuri ya kulima tangawiz na tangawiz inatoka kweli sio masihara ila kila msimu ni kupangiwa bei na hao wanao jiita ma Ajent , inafikia kipindi bei inapanda hadi elfu 3 kwa kilo lakin ni miaka hio watu walitajirika sana waliobahatika kwa kipindi kile bei ilivo kuja kushuka mpk elfu 1 hapo ni msim mzuri currenlty speaking bei asaiv ni mia 5, hili swala la kuexport ili ku cut down haw middle men lili kwepo way back na hii Post yako imeniamsha tena, ila nikifikiria mpaka iwe finished good in terms of quality wanayo taka wao (EUROP, US, etc) inahitaji KWANZA elim ambapo nina kadiploma kangu kutoka
(IFM) So masuala ya documentation nadhan hilo sio shida nikikomaa inawezekana, na PILI ni kamtaji kakubwa kdg na hapo ndipo napoishia kuweka wazo langu la biashara sijui mpk ln....???
 
Taasisi za bongo zipo vizuri kwenye kupiga fine na kuzuia tu na sio kutoa miongozo ya uboreshaji na kuongeza tija.
 
Hii ni kweli kabisa mtu wangu....umenena ninachokifahamu
 
Kufanya export ni jukumu zito kuliko ilivyo kawaida.

Kwanza inategemea unataka kufanya export ya kitu gani na mazao gani?

Ukiangalia, mazao kama pamba, tumbaku, kahawa, chai, cocoa na mengine mengi yameshikiliwa na wanunuzi wa kimataifa ambao, ndio wanamiliki soko.

Mfano, pamba ... Unaposafirisha pamba, mhitaji wa pamba ni mtengeneza nyuzi, au nguo katika viwanda , pengine Vietnam, India, Bangladeshi, Thailand na maeneo mengine.

Hawa wenye viwanda, hawanunui moja kwa moja toka kwa supplier/ toka nchi za kwetu. Ukitaka kuwauzia moja kwa moja, utapata ugonjwa wa moyo... Wao wana kawaida ya kubadilisha bei ya manunuzi kadri wanavyoona soko linavyofanya kazi kwa kipindi hicho.. Ukishindwa kukubaliana naye, basi utabakia na mzigo ... Na mara nyingi, bei zinaweza badilika mfano, umepakia mzigo bandari ya Dar es salaam na wakati unaelekea Malaysia, Singapore ili kupakia kwenye meli za mwisho kwenda kwenye , bei inabadilika na hiyo ndio bei mnunuzi atanunua nayo.. Haya mabadiliko ya bei kwa namna hii, itauwa biashara za wasafirishaji au wauzaji wetu wa Africa na nchi maskinii.. Utapata hasara kubwa ...

Hivyo kuepuka bei kubadilikabadilika wauzaji/ supplier wetu wanaingia mkataba na traders ( brokers) walioko ulaya na kwingineko kuwauzia pamba kwa bei ya kiwandani ( ex works ) au kuwauzia FOB Dar es Salaam port.. Sasa kama kuna mabadiliko yoyote ya bei, cotton traders ( brokers) wana uzoefu wa kushughulika na mambo hayo na wana uzoefu mkubwa, kwa vile wananua pamba maeneo mengi duniani.

Kuna watanzania nawafahamu, walijaribu kuuza pamba moja kwa moja , bila kupitia kwa madalali ( Brokers/ cotton traders) walipata hasara na hawakujaribu tena. Hasara ni kubwa sana, ukilinganisha bidhaa kama pamba ni thamani kubwa .

Haya yanafanyika katika maeneo ya mazao mengine na hizi huwa zinaitwa risk of international trade.

Ni hatua ya kimkakati na inahitaji uzoefu katika maeneo mengi..
 
Herr Muller naomba tuwssiliane my no. +255752406406
 
Mfano,jiulize una magunia 1000 ya maharage unataka upeleke Japan,je ni hatua zipi itabidi uzifuate ili mzigo ufiko unakotakiwa? je taratibu zote za kufuata zinakuwezesha wewe mzigo ufike kule bila wewe kuwa harassed?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…