cutelove
JF-Expert Member
- Oct 3, 2017
- 3,448
- 7,972
Ukubali usikubali lakini huu ndo ukweli wenyewe kuwa hakuna kitu kigumu kwenye maisha ya binadamu kama kulipa gharama za matibabu (kuuguliwa)
Kwa kweli gharama za matibabu Tanzania zipo juu sana na mtu binafsi anatakiwa alipe kabla ya huduma au kama huna bima
Yaani ukifika hospital uwe na hela usiwe nayo lazima ulipe kwanza mapokezi ndo huduma zingine ziendelee huku ukiendelea kulipa huduma ya kulazwa na vipimo mbalimbali na madawa
Ugonjwa haukwambii siku wala muda wa kuja kwenye familia yako wala haukwambii ni aina gani ya ugonjwa unakuja
Tunacheka vijiweni, sehemu mbalimbli lakini linapokuja suala la gharama za matibabu kwa sisi wenyewe tukiwa tumeugua au tumeuguliwa hapa watanzania hujikuta na msongo wa mawazo,na watu wengi wanapata stress kwa sababu ya kuuguza
Huku hela ya matibabu hapo hapo mgonjwa ale dah! Kwa kweli sio siri lazima uwe kichaa
Kwenye ugonjwa ndo watu wanajuta kuzaliwa,hasa unayeuguza,halafu binadamu tulivyo, michango ya harusi ipo fasta lakini kwenye matibabu simu hazipatikani,
Uzalendo ni kuwapenda watu wako,Watanzania ni masikini,bima ya afya kwa kila mtu mtawaokoa Watanzania wengi na stress za maisha
Kwa nini watanzania hatuna furaha, kwa nini tuna msongo wa mawazo ni kwa sababu ya kitu hiki
Watu watakwambia bora upatwe na tatizo lingine isipokuwa kuugua au kuuguliwa ,utajuta kuzaliwa,na watu wameuza rasilimali ,watu wamefilisika kwa sababu ya matibabu ,hata Bahati Bukuku analijua hilo
CHADEMA ikazie hiyo sera ya bima ya afya kwa kila mtu,hapo mmewagusa maisha ya watu tangu akiwa tumboni hadi uzeeni,bora umnyime mtu chakula lakini siyo matibabu
Kuuguza bila bima,Lissu okoa Watanzania