Kwanini Watoto wa siku hizi hawapendi kusoma?

SOCIOLOGISTTZ

JF-Expert Member
Joined
Jun 16, 2013
Posts
2,615
Reaction score
927
Jamani wadau naombeni jibu, watoto wa shule zetu siku hizi hawataki kusoma badala yake wanajishughulisha na mambo ya kihuni kama kuvuta bangi na kufanya mapenzi, na mambo mengine mabaya na kipuuzi wakiwa shuleni. Wazazi wanajitahidi sana kulipa ada na matumizi mengine wakidhani watoto wao wanasoma kumbe...

serikali ya CCM nayo inaongeza wastani wa kufaulu ili iyonekane imefanya mambo mazuri katika elimu.
nasema kweli bila ushirikiano wa waalimu, wanafunzi, wazazi na serikali shule zetu zitaendelea kufanya vibaya sana siku hadi siku, hata kama serikali ya ccm itaendelea kupanua magoli
.
 
Wewe unafikiri serikali ya ccm ni wajinga kiasi hicho wasome ili waelimike huwezi kuilinganisha elimu ya 1995 kurudi nyuma na ya sasa hivi uhuni mtupu enzi za mwinyi kwanza vijijini klabu za pombe zilikuwa zinafunguliwa saa nane mchana na ni sheria lakini siku hizi asubuhi unakuta vijana wadogo wanashinda baa kuanzia asubuhi mpaka usiku kunywa viroba na banana unatarajia nani atamfunga kengele mwenzie hapo.
 
Maana wanaiga vitu vyote hivyo kwenye jamii iliyowazunguka maana yke baba,mama,mjomba,shangazi,majirani,viongozi.
 
Cm,tv, serikali isiyo makini pamoja na msingi mbovu kuoka kwa wazazi ndio chanzo vyanzo vikuu
 
jf. Fesibuku, wasaPu, yutubu, wetwap, istagram,Na ikichangia elimu haina maana kwa hapa tizii hata usome mpaka univesiti lazima usote kitaa tu
 
Sisi wakubwa tunafanya nini juu ya hili???!!!!
Badala ya kuwalaumu na kuwashangaa tuchukue jukumu letu!!!!!!


Mabadiliko ni mimi,ni wewe, ni yule!!!!!
 
kweli OLESAIDIMU change ni sisi bila ya kupigania hili miaka ya baadae sijui itakuaje nahic tunaweza kuajiri watu akili zao hazipo kichwan zipo kwenye makaratasi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…