Kwanini Watu Hutuficha Baadhi Ya Mambo Yao

Kwanini Watu Hutuficha Baadhi Ya Mambo Yao

Etugrul Bey

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2020
Posts
6,514
Reaction score
15,247
Screenshot_20250102_144811_Google.jpg


Kwanza,wanatulinda tusiathirike na madhara yoyote ambayo tunaweza kuyapata baada ya kujua ukweli wa taarifa fulani fulani ambazo wao hawataki tuzijue,hivyo ni bora ikiwa hatutajua

Pili,wanatupenda,unajua kwakuwa wanatupenda hawapendi wawe mbali na sisi,wanafahamu kabisa mara baada ya kujua mambo yao hatutapenda watusogelee wala kuwa karibu na sisi,kwahiyo wakati mwingine ni bora kwetu kutoyafuatilia mambo yao

Tatu,hawataki tujue baadhi ya mambo yao,kila mtu ana uhuru wa kuwa na faragha yake,hivyo baadhi ya mambo hayafai watu wengine wayajue isipokuwa kwa wahusika tu

Nne,wanaogopa aibu ambayo wanaweza kuipata mara mambo yao yatakapo kuwa hadharani,kuna watu huko majumbani na makazini tunawaheshimu sana kwakuwa tu hatujui upande wa pili wa maisha yao,hivyo watatumia gharama yoyote kuficha mambo yao ili wasiaibike

Tano,wanaogopa kuharibiwa mambo yao au kudhurika,kuna watu ambao wakijua mipango yako na mikakati yako basi ujue umekwisha,watakukwamisha kwa namna yoyote ile,ili mradi wakuone hauvuki hatua moja na kwenda nyingine

Hivyo basi wakati mwingine tusilaumu na kulalamika kwanini watu wetu wa karibu wanatuficha baadhi ya mambo,jua kwamba ni kwa maslahi mapana undugu wetu na ujamaa wetu

Ni hayo tu!
 
Back
Top Bottom