Kwanini watu mjini wakipewa shikamo wanaitika 'salama za kwako'?

Kwanini watu mjini wakipewa shikamo wanaitika 'salama za kwako'?

Pdidy

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2007
Posts
57,951
Reaction score
32,619
Habari zenu wakuu hapa kati na kakazi hapa posta nafanya

Yaani unakutana na kabinti kazuri kanakusalimia shikamoo

Wale wazee wanajibu salama za kwako, hivi mmelogwa

Mi kijana naitikia marahaba we unakataa shikamoo unataka nini tena?

Hizo tabia muache wengine tuna watoto wa kike mtatuogopesha tukisikia wanafanya kazi mjini..

Inaendelea.....
 
Salamu ya kinafki sanaa inamfanya mpokeaji aanze kujitafakari mpaka huyu ananisalimia wengine mamiili jumba umri punje alafu unamsalimia mtu mwili punje umri jumba ataitikia kwa bashasha kwelii?
Shikamoo mwisho 25yrs ukivuka hapo salimia wazee wenzio habari inatosha.
 
Sasa na wewe ni kwanini uandike kwa herufi kubwa kama vile unajaza fomu ya NIDA?
 
Salamu ni ishara ya heshima hutolewa kutoka kwa mdogo kwenda kwa mkubwa kuashiria heshima na nidhamu kwa mkubwa

Sasa unakuta mtu tu alivyovaa hana adabu wala heshima anakusalimia shikamoo yanini?

Au anaeamkiwa mwenyewe hajajiweka kiheshima unamuamkia wakazi gani

Sisi huku vijijini tunapigana kwa kugombania heshima wadogo lazima watusalimie hata kama nimekupita lisaa
 
Hawataki kuitwa babu "Babua za kwako za kwangu nikaangie".
 
Watu wa mjini wanapenda kujidogodisha sana, unakutana mjimama huo mdingi huoo halafu unaniambia shkamoo mmh hapana jamani hapana.
 
Hili tatizo Kwa Dar es salaam limekuwa sugu.yaani unamuona jimama lizee kabisa unampa shikamoo anakuitikia kwemaaa?Kwa Sasa Mimi hata kama ni mzee namsalimia habari mzee?nitawapa shikamoo wazee wangu pekee wa kunizaa.
 
Shikamoo ni salamu ya kitumwa tumwa
 
uwe unawaamkia ‘Babu mambo vipi’ ‘Mama niaje?’

wanapenda sana ilihali unatumia prefix kama Babu,Bibi, Dada , Kaka
 
Uzee mwisho.... niliwahi kusikia kauli kama hii ikitajwa kipindi cha nyuma.
 
Huto tudemu twenyewe twa 2000 tunapenda sisi wazee acheni wivu madogo
 
Back
Top Bottom