Naombeni jibu tafadhali. Unakuta ndugu/rafiki anaumwa hakuna mtu anaeonekana kusaidia ILA subiri kama mgonjwa akifariki yani hapo watu wanataka kuonyesha uwezo wao.
Nadhani hapa unaongelea wanandugu, maana ndio wanaopata taarifa za ugonjwa!
Otherwise, kwa watu wengineo ni jambo la kawaida kuchangia kumpuzisha marehemu~!
Watanzania ni maarufu sana kwa majigambo ya tabia wasizokuwa nazo. Ni rahisi sana kusikia watanzania ni wakarimu na wanapendana lakini ukifuatilia kwa undani utajua kwamba kinachosemwa ni kinyume. Hebu fikiria
1. Umewahi kufananisha kiasi cha mchango mtu anachotoa kwa ajili ya harusi na sherehe zingine na support ya watu halafu ukalinganisa na muitikio wa watu kama utaomba msaada wa ada ya shule?
2. Umewahi kujiuliza kwa nini mtu yuko radhi akununulie hadi creat ya bia lakini ukimuomba ile hela ya bia akupe atakukatalia!
3. Umewahi kumleta ndugu yako halafu ukampa kitengo badala ya kukiendeleza anakifilisi?
4. Umewahi kujiuliza kwa nini mtoto wa kike wakitanzania ni kawaida kuzalia nyumbani ili mtoto atunzwe na bibi na babu? Katika hayo yote utagundua ni muendelezo wa roho za kuzuiana kuendelea.''Michango ya harusi inaisha kwa siku mojakwa hiyo hutajenga nyumba. Ukinywa bia utalewa lakini nikikupa 20,000 unaweza kwenda kuanzisha biashara ya nyanya ukafanikiwa. Ukinipa biashara yako maana yake wewe una hela nyingi utapata zingine.Ni wajibu WENU baba na MAMAkunitunza mimi na mtoto wangu!" HUU NDIO UJINGA UNATUFANYA WATANZANIA TUTAKUWA MASKINI MILELE KWA ROHO ZETU MBAYA!
watanzania wengi wanapenda kufanya vitu vitakavyowaonyesha yaani wanapenda sifa,ndio maana kwenye misiba na hata kwenye vikao vya harusi michango kibao,lakini kumchangia mgonjwa hawapendi nani atawaona