Kwanini watu tunapenda kuamini vitu tusivyovijua?

Kwanini watu tunapenda kuamini vitu tusivyovijua?

de Gunner

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2021
Posts
2,044
Reaction score
4,558
Sema kweli mimi huwa nashindwa kuelewa watu, nashindwa kabisa sometimes hata kuchangamana na aina flani ya watu kwasababu najua tu hawana manufaa. Sipendi kuongelea watu na kujudge wafanyacho, ila percent kubwa ya watu wanizungukao huishi hivyo

Hii hunipelekea kuwa mpweke mda mwingi ila nashukuru mungu sijihisi hivyo sikuhizi. Jamii imejaa watu wanafiki, wambea, wasio na upendo kwa wengine. Wanaishi na wengine kwa maigizo yaani asubuhi mnasalimiana fresh then ukimpa kisogo anakusema vibaya. Hasa majirani, hawa ndo wanafiki wakubwa kama upo huna shobo wala huna mazoea sana, watakutakazia maneno mtaani ili na wengine wakuone mbaya japo huna shida kabisa.

Sasa ubaya ni kuwa hayo maneno unayopakaziwa siyo ya kweli na hakuna ushaidi wowote lkn watu huamini na kuanza kukuona katika mtazamo huo wa kusikia maneno ya watu, ambayo yamejaa chuki na visa visivyo na ukweli wowote. So hii inapelekea wengine kukuchukia bila sababu. So, huwa nashindwa kuelewa sijui ni kwa nini binadamu tuko hivyo, kwa upande wangu sijawahi kuamini stori kuhusu mtu mpk niishi nae nijue mwenendo wake ndo nipate majibu kamili, ila watu hasa sisi wabongo sijui tuna nini unakuta mtu anaku avoid na hujamfanya kitu wala kumsemesha vibaya ila unajiongeza tu kuwa tyr wamesha mpakiza maneno.

Kingine kwanini mtu asiyependa uongo na umbea huchukiwa? Meaning mtu ambaye hujali mambo yake na kuishi kwa usawa bila ku favour upande mmoja kwa nini watu wa aina hii hutengwa. Utaskia yule anajiona kweli, sjui anajifanyaga mjuaji maneno lukuki ili kuwafanya wengine nao wakuchukie, na wenyewe bila kuchunguza wanakubaliana nao tu.

Sisemi watu wote wapo hivyo ila jamii imejaa watu wengi wa namna hio waongo, wachonganishi, wenye wivu na chuki binafsi. Ukweli hili swala kwa wenzetu lipo ila sio kama huku bongo. Yaani linakera sana.
 
Upo sahihi mkuu, bahati mbaya ndio dunia ilivyo espicially hii dunia ya tatu!
 
Back
Top Bottom