Uchaguzi 2020 Kwanini watu wanalazimishwa kucheka ilhali mioyo inalia?

Uchaguzi 2020 Kwanini watu wanalazimishwa kucheka ilhali mioyo inalia?

Mikono yenye Sugu

Senior Member
Joined
Jul 1, 2020
Posts
133
Reaction score
215
Nakipenda chama changu (CCM), lakini kinaniangusha pale tunaposhindwa kuzijibu hoja za wapinzani wetu na badala yake tunawalazimisha kutusifu na kuonesha nyuso za ucheshi, bashasha na tabasamu ilhali mioyo yao inalia.

Nashauri tuzijibu hoja zao bila kejeli, hasira wala kuwatumia vyombo vya mabavu kuwanyamazisha. Naamini majibu tunayo na wenye kutafakari ukweli watatuelewa na kutupokea.

Upinzani sio hatia, usaliti wala dhambi, na kamwe upinzani hautamalizika kwani hata MWENYEZI MUNGU mwenyewe alimwacha shetani awepo ili wasiomkubali yeye nao wawe na kiongozi wao.

Ee chama changu, tusiwe chanzo cha Watanzania kugawanyika bali chanzo cha wao kuwa na mshikamano na umoja wa kitaifa. Hiyo ndio ilikuwa njozi ya Mwalimu Nyerere na wenzake walioliasisi taifa hili.

MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WATU WAKE!
 
Umesema vizuri.Wametulazimisha hata sisi hambao hatukustahili kusikiliza matusi, sasa tunayasikia. Sijui wanatupeleka wapi hawa?
Umri wa kupiga kura.jpg
 
Huu ujumbe Polex2 na team yake waupitie.
 
Huwa bado najiuliza ni kwa nini sasa hivi kila mtu anahisi ana akili kuliko mwenzie?
Sasa ona mtu anajuaje kuwa fulani analia moyoni, ilhali ya moyoni ni siri?
 
Siku zote furaha ya shetani ni kuona watu wanateseka
 
CCM ni vizuri wakajitafakari.. watanzania wanajilazimisha tu kucheka ila kiuhalisia HOI kimaisha.
 
Back
Top Bottom