Kwanini watu wengi huogopa Hesabu?

TGInnocent

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2013
Posts
1,088
Reaction score
582
Watu wengi niliosoma nao tokea shule ya msingi mpaka chuo wamekuwa wakiogopa sana kujihusisha na michepuo ya masomo ambayo ina hesabu kwa wingi, au ikitokea somo la hesabu ni lazima katika mchepuo huo, hufanya vibaya sana katika somo hilo.

Rafiki mmoja alitutania kwa kusema yeye amependelea kusoma mambo ya sheria kwa vile huko namba hazina nafasi kabisa kiasi kwamba hata orodha ya vitu hutamkwa kwa kutumia herufi badala ya namba, mfano a, b, c, na kuendelea badala ya 1, 2, 3, na kuendelea.

Nijuavyo mimi kujua hesabu ni moja ya nyanja muhimu ambayo bila hiyo elimu kwa ujumla wake yaweza kuwa duni. Hesabu hupanua sana uwezo wa kufikiri na kujenga hoja za kisayansi na kijamii. Mfano hesabu za "logic", "probability", "statistics", maumbo n.k. zote zina nafasi pana ya matumizi katika kila idara iliyo kwenye mifumo yoyote ile ndani ya jamii, hii ikiwa ni pamoja na mahakama, hospitali, familia, biashara, kilimo, michezo, n.k.

Ikiwa tatizo hili linaendelea kwa vizazi vyetu vya leo tutambue kuwa watoto wetu na vizazi vijavyo vinaweza kugubikwa na taifa lenye watendaji wengi wenye uvivu wa kufikiri na matokeo yake ni kudidimia zaidi kwa maendeleo ya nchi yetu.

Natia shaka kuwa, yawezekana kabisa utendaji mbovu wa uchumi katika nchi yetu unatokana na watendaji wengi katika sekta mbalimbali kuwa na uelewa mdogo sana (ukilaza) wa somo hili la Hesabu na hivyo kushindwa kulitumia ipasavyo. Hebu sema ni jambo gani haliwezi kutumia hesabu ili kusaidia kufanya maamuzi bora?

Natoa mtihani mdogo sana hapa kwa wanaJF kupima 'vilaza' wa hesabu (usikwazike, sijatukana). Kokotoa na kuweka jibu la swali hili dogo, samahani sijaweka 'multiple choice' na kisha changia mada katika kutoa ushauri nini kifanyike kuhamasisha vijana mashuleni na vyuoni kupenda Hesabu.

Swali: Pande mbili za sambamba trapeza zina urefu wa sm 5 na sm 8. Ikiwa umbali kati ya pande hizo ni sm 10, kokotoa eneo la trapeza hiyo.

Tahadhali: ukijibu na kukosa ni kilaza, usipojibu hujui.
 
Pande mbili za sambamba trapeza !? kwanza ni mara yangu ya kwanza kusikia jina la umbo hili "sambamba trapeza"! kwa umbo kama hili najua tu utanichukulia kuwa sijui maana sitajaribu kulijibu. Labda ulisuke upya kisha ulilete tena.
 
Hawajui kutokana na walimu wengi kuwa discourage na kuwa wakali pia na dhihaka kama ulivyofanya wewe hapa kumwita MAVUNO kilaza matokeo yake mtu anakuwa anaona aibu kutaka kujifunza. Btw ni watanzania wachache sana hawajui hesabu hivyo sidhani kama uzi wako una ukweli
 
Last edited by a moderator:
Alieleta thread hii mwenyewe ni dhaifu. msikute mnajibishana na mtoto wa form two ambaye kaiacha simultaneous juzi, sasa komaeni kumjibu tu.
 

Soma mada ili kujua sababu ya Mavuno kupata hiyo category ya 'kilaza'. Kimsingi hajaweka jibu sahihi.
 
Last edited by a moderator:
Alieleta thread hii mwenyewe ni dhaifu. msikute mnajibishana na mtoto wa form two ambaye kaiacha simultaneous juzi, sasa komaeni kumjibu tu.

Changia mada kama una ushauri wowote, kumbuka sio lazima kukokotoa swali endapo unaogopa kuanika ukilaza wako wa hesabu hadharani.
 
Alieleta thread hii mwenyewe ni dhaifu. msikute mnajibishana na mtoto wa form two ambaye kaiacha simultaneous juzi, sasa komaeni kumjibu tu.

Mbona ww tyr umeshachangia? Kam unaon n mtt wa form two si ungepiga kimya??
 
Mleta mada pia ni kilaza
Ameuliza swali akiwa hajui anataka nn
 
Trapeza ina pande mbili sambamba moja huwa kubwa zaidi ya nyingine Pia huwa na kimo ambacho ndiyo umbali kati ya pande hizi mbili sambamba.
Na katika kutafuta eneo la trapeza Huusisha pande mbili ambazo ni sambamba na kimo.

Eneo=0.5(a+b)xh

a upande mdogo/mfupi

b upande mkubwa/mrefu

h kimo.

Kwa uelewa wangu mdogo wa mathematics.
 
Soma mada ili kujua sababu ya Mavuno kupata hiyo category ya 'kilaza'. Kimsingi hajaweka jibu sahihi.

Najua hajaweka jibu sahihi ndio maana akaitwa Kilaza, concern yangu ni maneno kama hujui, huna lolote au kilaza ndio yanamfanya mtu awe mwoga, suruhisho hapo angempa njia ya kufanya au kumuuliza amefanyaje na ndio maana inapokuja suala la hisabati hata kama mtu atakosa jibu kuna maeneo kama alikuwa ana flow nzuri kuelekea kwenye jibu unakuta anapewa maksi.

Mie niliwahi kutolewa mbele na mwalimu wa hisabati ku-solve simultaneous equation by substitution long kitambo nikiwa form 2 nikashindwa na mwalimu alikuwa mnoko na akanitolea dhihaka ya "mwenyewe umetoka nyumbani na shati lako zuri umeliwekea blue na kuchomekea shati alafu umeshindwa ku-solve hilo swali, bure kabisa" unajua nilikosa ujasiri kabisa na nikaanza kukichukia kipindi chake,

kilichoniokoa nilikuwa nina background nzuri ya hisabati primary school pia nilikuwa nasoma masomo ya sayansi hivyo kulikuwa hakuna jinsi lazima nihakikishe nakomaa nayo.
 
Kila kitu hejengwa,wengi shule zao hazina walimu wanaoweza kufundisha mwanafunzi vizuri.
 
Pole Jodoki, lakini bado tunapaswa tufikirie ni jinsi gani tufanye vijana wetu walipende somo hili bila kujali vikwazo kama ulichokutana nacho. Kumbuka hata maisha nayo huwa hostile sana lakini hayatuzuii kupambana nayo.

Wakati mwingine kejeri, viboko, kubezwa zaweza kuwa nguvu za kutuchochea kufanya vizuri.
 
Mavuno kwanza usikasilike kwa kukuita kilaza, hiyo ilikuwa ni tahadhali iliyotolewa kwenye swali kwamba ukijaribu na kukosa jibu sahihi basi unakuwa kilaza, vinginevyo hujui. Sasa maelezo yako ni sahihi kabisa ila jibu ulilolitoa haliko sahihi.

Tunajifunza hapa kufungua ufahamu na kudadisi kwa nini nimekosea badala ya kung'ang'ania vile tunavyoona. Ukifikiri kidogo tu utaona kuwa kweli jibu ulilotoa sio sahihi, hii huwafanya vijana wengi watoke kwenye mitihani yao wenye furaha lakini matokeo yakisomwa, looo hawakufaulu.
 
Kila kitu hejengwa,wengi shule zao hazina walimu wanaoweza kufundisha mwanafunzi vizuri.

Waballa, unatoa ushauri gani kutatua hilo tatizo ulilolibaini la kutokuwepo walimu wenye uwezo wa kufundisha somo la hisabati.
 
solution
1/2×(3×10) +(5×5)=40
~=40 sm square
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…