Kwanini watu wengi huvutiwa na umbea?

Msingi_Kiuno

Member
Joined
Feb 22, 2017
Posts
86
Reaction score
126
habar yenu nyote wakuu...

nawaalika nyote tumulike kwa kujadiliana, ni sababu zipi zinapelekea watu wengi kuvutika na habari zisizo na mashiko ktk kubadili maisha yetu kiuchumi.....

wanaouza habari za uwekezaji, uchumi, biashara nk wanapata soko kwa tabu sana.

ila habari kama za udaku, umbea, vichekesho na zifananazo na hizo hubamba haraka sana.

nini hasa kinatufanya binadamu kuwa hivyo?

karibuni nyote....
 
Mm pia nataman kujua sijui kuna nguvu gani nyuma ya mambo kama hayo kupendwa zaidi na walio wengi.
 
Ni kwa sababu binadamu tunapenda kuchunguza na kuyajua ya watu kuliko yetu binafsi
 
Fikiria mtu katoka kazin amefokewa na boss, nyumbani wife au husband kawa pilipili watoto ada hujui utaipata vipi utataka tena kusikiliza habar za uwekezaji?

Bora ujue ya Bashite uongeze siku

wanaouza habari za uwekezaji, uchumi, biashara nk wanapata soko kwa tabu sana.
 
Fikiria mtu katoka kazin amefokewa na boss, nyumbani wife au husband kawa pilipili watoto ada hujui utaipata vipi utataka tena kusikiliza habar za uwekezaji?

Bora ujue ya Bashite uongeze siku
ha ha ha haaaa........ mbavu zangu mie. kwaiyo umbea unapunguza stress kwa kutoa faraja nafsini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…