Samcezar
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 13,095
- 22,731
Habarini.
Kuna ile hali ya baadhi yetu, huwa katika kila mahusiano mapya unaingia unajikuta hayadumu hata ukijitahidi kuwa vizuri maeneo muhimu. Na hata ukijituma bado utajikuta ndani ya huo uhusiano amani inakuwa haipo na utulivu unakosekana.
Mojawapo ya sababu ni mahusiano tuliyokuwapo awali na namna tulimalizana vipi na hao tuliokuwa nao awali. Kuna wale wenza huwa tunaachana nao na wanatuacha na kifungo cha lawama. Walokole wanaita laana.
Hapa sizungumzii wale Ma X tulioachana nao tukicheka na utani mwingi. Nazungumzia yule binti uliyemtoa bikra na kumuahidi kuwa utakuwa nae then ukamuacha solemba ile hali ndani ya moyo wake bado anakupenda na amepigwa butwaa unakwenda wapi ukimuacha pekee yake.
Nazungumzia yule kijana aliyekupenda kwa dhati akijitoa kwako na kukupatia kila kitu kipindi akiwa yupo chini kimaisha ila wewe ukaona umpe huo mwili wako na maisha yako yule kaka akiyetengana na mke aliyezaa nae watoto wawili kwa kufuata ushauri wa shoga zako au mama yako au wazazi wako ambao walitazamia maslahi na sio utu.
Wa tu unaowaacha kwa maamuzi yako binafsi huku wao wakistaajabu ni kwann umeamua maamuzi hayo, huwa roho zao hujikunja mara tu wanapopata taarifa kuwa kuna mtu mpya kwenye maisha yako na hukosa cha kufanya na roho zao hujikunja na kukufungia wewe huko uendako.
Unaweza kudhania haya ni maneno matupu ila chunguza utakuja nambia.
Mtu asiye na hatia roho yake inapofunga kisasi huwa kinafanywa na malaika wa maumivu. Wewe utahisi upi salama na vitu vitakwenda vizuri kwa muda mrefu sana hadi pale shimo ulilotumbukia liwe na kina kirefu sana cha wewe kushindwa kutoka ndipo malaika wa kisasi huanza kazi yao.
Kama ni mume wa mtu utashangaa ghafla familia yake imerudi kwenye maisha yake kwa kasi. Kama ulichezea binti wa mtu na kumtoa usichana kisha ukamtosa jiandae huko uendako, mkeo, na watoto wako, kile ulichomfanyia mwenzako utakiona na kwako pia.
Whatever u do. Usijemuumiza mtu moyo kwa makusudi bila kosa lolote. Kama unajua unataka starehe tafuta bedui mwenzako mkafanye yenu, kama unajua unatafuta mapenzi ya dhati then kuwa serious na moyo wa mtu asiyekuwa tayari kwa michezo.