Kwanini watu wenye mtindio wa ubongo huwa wanafanana kwa kiasi kikubwa?

Twinawe

JF-Expert Member
Joined
Oct 3, 2016
Posts
2,431
Reaction score
5,336
Habari ndugu zangu sipo hapa kudhihaki wala kukosoa uumbaji wa Mungu au kumtukana yeyote kwa namna yeyote ile naomba atakayekwazika na swali langu anisamehe ndugu zangu.

Nimekuwa nikijiuliza, kwanini hawa watoto au watu wenye mtindio wa ubongo /matatizo ya akili kwa kiasi kikubwa sura zao huwa zinafanana haijalishi ni ke au me?

Ukiangalia wengi wana macho makubwa na nywele kama za kisomali. Kwanini iko hivyo na ufanano wao unatokana na nini mbona sio kama vichaa(Vichaa hawafanani kila kichaa yuko kivyake)?

Nakaribisha maoni wadau naamini wenyeji wa Kilimanjaro mtakuwa mashahidi kwa hili especially maeneo ya vijijini ndo wapo kwa wingi kulinganisha na sehemu yoyote Ile.
 
Kuna wale utaahira wao unatokana na hitilafu za DNA ugonjwa unaitwa downs syndrome hawa wanafanana vichwa vidogo macho yalotokeza na mengine ulioyasema
ila utaahira unaotokana na external factor kama ajali, kurogwa na kadhalika huwa hawafanani.
 
Ehe
Kwanza naomba ubadili Lugha
Hakuna mtu anaitwa taahira wala zezeta wanaitwa wana mtindio wa ubongo/matatizo ya akili

Kuna makundi mengi ya matatizo ya akili Mfano
1. Mental retardation/
2. Autism
3. Down syndwon
4. Celebral palsy na
5. ADHD

Kundi unalo zungumxia wewe ni Down syndrome
Hawa wanasura za kufanana pia ni za mviringo (round face)

Hii ni aina ya ulemavu wa akili ambayo inatokana na sababu mbali mbali
Mfano . Inheritance, genetic malformation, nutrition, matumiz ya vilevi na cigarette, nk...

Kiufupi hata wewe unaweza kuzaa mtoto wa aina hii
 
Ndo maana ayo maneno niliyaweka kwenye mabano sababu huku mtaani wengi tumezoea kuwaita hivyo wengine wanawaita ndondocha ni maneno yasiyo rasmi neno rasmi ni mtindio wa ubongo nimeliweka
 
Labda mazingira yao wanayoishi yatakua na mchango katika hilo
 
Downs syndrome husababisha na external factors ambazo husabisha sudden change in displacement of gene during gamete formation kipindi hiki kwa wale watumizi wa technolojia za mawasiliano kupita kiasi kama computers and mobile phone wanaweza kuwa hatarin kwa hili swala if radiations emmited are exposed to the reproductive organs(for male)
 
Hapo awali watu hao waliitwa "Mongoloids" kwa jinsi walovyofanana na watu waishio Mongolia. Kwa vile jina hili lilikuwa linawadhalilisha watu wa nchi hiyo liliondolewa na sasa wanafahamika kama waathirika wa Downs Syndrome
 
Sio neno zuli kwa kulitumia kuwaita mataahira tumia utindio wa ubongo.
 
Kweli wanafanana hapa Jirani tunae watu wanatumia madhaifu yake kumpinda na hana siri anapenda kuomba pesa ya kununua vitu kababu n.k Leo nimepata elimu mpya viva jf
 
Taahira ni neno la kiswaili tusipende kutupa lugha yetu kinafiki kwakutumia lugha za wengine sidhani kama ayo majina ya kingereza ulitaja hapo hakuna kiswaili chake cha moja kwa moja.

Kukwepa lugha yetu ni utumwa mbaya zaidi Kama tunaona jina la lugha yetu ni baya masikioni mwetu dawa nikutafuta jina jingine nasio kufunika funika mambo kinafiki wakati ayo majina tunayoyakwepa hayabadilishi maana au tatizo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…