Kwanini watu wenye vyeo, elimu na madaraka hawapendi kukosolewa na walio chini yao, hata wanapokuwa na makosa?

Joined
Oct 5, 2026
Posts
31
Reaction score
51
Habari za muda huu wanaJF.

Kuna jambo ambalo nimekuwa nikilitafakari katika jamii yetu. Mara nyingi, baadhi ya watu wanapopata vyeo, elimu ya juu, taaluma au mamlaka fulani, huonekana kuwa na wakati mgumu kukubali wanapokosolewa na watu wanaowaona kuwa wako chini yao.

Kwa mfano, mwalimu anaweza kukataa kukosolewa na mwanafunzi hata pale mwanafunzi anapokuwa na hoja ya msingi. Daktari anaweza kupokea vibaya maoni ya mgonjwa au ndugu wa mgonjwa. Vilevile, kiongozi anaweza kuona kama amedharauliwa anapohojiwa na mtu wa kawaida.

Swali langu ni hili: Je, kuwa na elimu, cheo au mamlaka kunamfanya mtu ajione kwamba hawezi kukosea?

Ninaelewa kuwa uzoefu, taaluma na nafasi ya mtu vinastahili kuheshimiwa. Lakini je, heshima hiyo inapaswa kumaanisha kwamba mtu huyo asikosolewe kabisa?

Kwa mtazamo wangu, kukosolewa si lazima kumaanishe kutoheshimu mtu. Wakati mwingine, anayekosoa anaweza kuwa anajaribu kurekebisha kosa, kuzuia madhara au kutoa mtazamo ambao mwenye mamlaka hajauona.

Hata hivyo, kuna tofauti kati ya kukosoa kwa nia njema na kumdhalilisha mtu. Hoja yangu inalenga zaidi pale ambapo mtu anakosolewa kwa hoja za msingi, lakini badala ya kujibu hoja hizo, anatumia cheo, taaluma au mamlaka yake kumdhibiti anayemkosoa.

Maswali kwa wanaJF:

1. Kwa nini baadhi ya watu wanapopata vyeo au nafasi za juu huwa na ugumu wa kukubali kukosolewa na walio chini yao?
2. Je, tatizo ni kiburi, malezi, mfumo wetu wa kijamii au namna tulivyozoea kuheshimu mamlaka?
3. Mwanafunzi akimrekebisha mwalimu kwa hoja sahihi, au mgonjwa akitoa maoni yenye msingi kwa daktari, je, wanapaswa kupewa nafasi ya kusikilizwa?
4. Tunawezaje kujenga jamii ambayo mtu anaheshimiwa kwa nafasi yake, lakini bado anawajibika kwa makosa yake?

Ningependa kusikia mitazamo yenu, hasa kutoka kwa walimu, madaktari, viongozi na watu wengine wanaofanya kazi katika taaluma mbalimbali.

Je, cheo kinapaswa kumpa mtu mamlaka ya kuongoza tu, au pia kinampa haki ya kukataa kukosolewa?
 
Samuya ana elimu mbalimbali na hataki kukosolewa na waliomzidi elimu.

Leo anataka kumyonga Tundu Lissu huku akitaka kumfutia uwakili Mwabukusi wakati mwenzake amekaa darasani, hajafika pale kibahatibahati
 
... ukiacha wenye sifa ulizotaja, ni watu gani wanapenda kukosolewa na wa chini yao?
 
"...nina degree nne kutoka nchi mbalimbali,naanzaje kuambiwa cha kufanya na aliyeishia la saba B?" Harrison.
 
Nadhani mfano halisi ni baba yako. Je anakubali kukosolewa? Kuepukana na ubishi usio na maana, we mkubalie tu hoja yake ili maisha mengine yaendelee.
 
... ukiacha wenye sifa ulizotaja, ni watu gani wanapenda kukosolewa na wa chini yao?
Ndiyo maana hasa nataka kufahamu, shida huwa nini? Kwa nini baadhi ya watu wanapokuwa kwenye nafasi za juu huwa hawapendi kukosolewa na walio chini yao? 🤔 Cha kushangaza, hata wanasayansi hukubali kukosolewa na watafiti wenzao, na wako tayari kurekebisha mawazo yao pale wanapoonyeshwa ushahidi wenye mashiko. Kwa nini basi katika baadhi ya mazingira, cheo au nafasi ya mtu inaonekana kuwa kikwazo cha kukubali kukosolewa na mtu wa chini yake? Je, tatizo ni mfumo tuliojenga, malezi au namna tunavyoelewa heshima na mamlaka?
 
Nadhani mfano halisi ni baba yako. Je anakubali kukosolewa? Kuepukana na ubishi usio na maana, we mkubalie tu hoja yake ili maisha mengine yaendelee.
Nakubaliana na wewe kwa kiasi fulani mkuu, lakini je, kukubali hoja ya mtu ili kuepusha ubishi ni sawa na kukubali kwamba hoja yake ni sahihi? Vipi kama hoja yake ina makosa na wewe unayajua, utakubali tu kwa sababu ni baba yako au mtu mwenye mamlaka kuliko wewe? Mimi nataka kuelewa kwa nini baadhi ya watu huona kukosolewa na walio chini yao kama dharau, badala ya kuangalia kama hoja iliyotolewa ina ukweli au la. 🤔
 
Tumia ukosoaji usio wa moja kwa moja. Huo wa moja kwa moja inatafsiriwa ni dharau.
 
Nadhani swala muhimu hapa ni kujua namna ya kutoa mawazo yako, au kufikisha ujumbe wako au kujenga hoja mbadala, au kushawishi mtu akubaliane na hoja yako bila kumkwaza.

Cha kwanza kabisa inabidi uondoe neno kukosoa Kichwani mwako. Hauhitaji kumkosoa mtu mwingine. Kila mtu ana fikra zake na mtazamo wake juu ya jambo fulani, hivyo ni lazima umuheshimu kwa hilo.

Unachohitaji ni kumshawishi akubaliane na hoja mbadala au mawazo mbadala ambayo wewe unayotoa.

Ukisoma kitabu cha Dale Carnegie How to Win Friends and Influence People anajaribu kutoa mbinu mbalimbali na approach kuhusu hili jambo.
 
Wala siyo watu wote wenye hizo factors Tatu, elimu, madaraka na vyeo...Kuna wengine hawana kabisa hizo factors mbili au Moja au hawana kabisa but still hawataki kukosolewa.. kwaiyo hulka ya kutotaka kukosolewa ni tabia ya asili ya Binadamu inayotokana na nguvu ya utawala.
 
Hii imejengeka kwenye tamaduni zetu. Anzia nyumbani tu wazazi hawataki kukosolewa na watoto je hao wazazi wakipta fursa ya kuongoza nchi watakubali kukosolewa. Mama anafanya uninga mtoto akisema anatishia kumpa laana eti kisa alimbeba tumboni miezi 9 na kumnyonyesha.

Acheni kuwalaumu viongozi waliotengenezwa na tamaduni zetu za kijinga za kutokutaka kukosolewa. Nyie mnaosema viongozi hawataki kukosolewa mkikosolewa mnatukana na kuwaita wengine machawa.

Tamaduni zetu zimetengeneza watu wasiopendankukosolewa acheni kulaumu viongozi
 
Baba wa familia tu, hataki kukosolewa na mke wake wala watoto, Hii ipo sana kwa Ngozi nyeusi.

Utasikia, mimi ndo kichwa cha familia, na nishafanya maamuzi 😀.

Kmmke.
 
Kuna DG mmoja si vyema kumtaja humu ilikuwa kwenye meeting na wafanyakazi akapewa kama ushauri haikuwa kukosolewa kabisa basi aliongea huyo acha kabisa huku akihoji wewe una elimu gani, baada ya kikao kuisha aliitisha jopo la wataalamu wamshauri nini kifanyike kulikuwa na changamoto fulani basi akaita wahandisi wakajadiliana sana wakamshauri ila kuna technician ana uzoefu sana na swala hilo na ndiye mtaalamu pia akasema basi aitwe tusikie atashauri nini, kuitwa anashangaa jamaa yule yule ili kuondoa aibu akamwambia unajua pale hukufata utaratibu unaotakiwa kwenye maongezi ila kwasababu mkubwa hakosei jamaa akajikalia kimya.

Wengi wao wana Ego ila kuna wengine kiukweli unaweza usiamini kabisa kama mkubwa vimbelembele na wenye dharau ni hawa wasaidizi wa HR, Maafisa utumishi au Administrative officers (AO) ni kama ofisi za baba zao.
 

Kwa uzoefu wangu, Ego doest pay.
 
Hasa tamisenga
 
Tabia ya kutokutaka kukosolewa ipo africa na nchi za ukomunisti.
 
Ukishasema kukosolewa-tayari umeshaharibu. Kumbuka Mkubwa /Kiongozi hakosolewi bali anashauriwa.
2. Je, tatizo ni kiburi, malezi, mfumo wetu wa kijamii au namna tulivyozoea kuheshimu mamlaka?
Kumbuka kwamba Kile unachomshauri a.k.a kumkosoa, Yeye ndo atawajibika endapo litatokea Tatizo au Changamoto kubwa kwenye utekelezaji.
Kwa hiyo ni lazima awe mwangalifu sana sio kupokea kila hoja inayoletwa kwake.
3. Mwanafunzi akimrekebisha mwalimu kwa hoja sahihi, au mgonjwa akitoa maoni yenye msingi kwa daktari, je, wanapaswa kupewa nafasi ya kusikilizwa?
Ni sahihi. Wanapaswa kupewa nafasi ya kusikilizwa lakini sio kutekeleza 100% kama walivyolileta kwa kiongozi.
Halafu kuna namna ya kuwasilisha hoja kwa kiongozi wako. Hoja nzuri ikiwasilishwa kwa njia sahihi na muda muafaka huwa ni nzuri sana kwa kiongozi kuitafakari na kuona namna kuifanyia kazi. Usipeleke Hoja yako kwa mtindo wa "Kufoka" au Kiongozi amekabiliw na jambo zito halafu na wewe anakandamizia la kwako. Anaweza kukutimua ofisini kwake.
4. Tunawezaje kujenga jamii ambayo mtu anaheshimiwa kwa nafasi yake, lakini bado anawajibika kwa makosa yake?
Ni suala la Elimu ya Ufahamu (Awareness)kwa pande zote husika.
Ningependa kusikia mitazamo yenu, hasa kutoka kwa walimu, madaktari, viongozi na watu wengine wanaofanya kazi katika taaluma mbalimbali.
Oooh! Mi sio mmoja wapo wa hao uliowataja ila ni Mdau mchangiaji tu. Au na wewe unanikataa kwakuwa sijatimiza Vigezo na Masharti?
Je, cheo kinapaswa kumpa mtu mamlaka ya kuongoza tu, au pia kinampa haki ya kukataa kukosolewa?
Cheo kinampa mtu mamlaka ya kuongoza au Kuwa ndiye mwenye kauli ya mwisho katika Maamuzi hata kama maamuzi hayo ni collective yeye ndo atabeba dhamana.

Hili ni Swali/Hoja nzuri sana.
Nachangia kama ifuatavyo: ref kila swali na mchango wangu hapo juu. Asante.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…