Kwanini wawekezaji wasipewe sekta zilizoshindwa kusimamiwa?

Kwanini wawekezaji wasipewe sekta zilizoshindwa kusimamiwa?

MDAU TZ

Member
Joined
Jun 9, 2023
Posts
12
Reaction score
53
Habari wana JF,

Binafsi napata mkanganyiko wa kimawazo kwa kuona Taifa kubwa kama TZ linashindwa kusimamia secta zake muhimu kama bandari na kuamua kutafuta wabia,kwa wakati kama huu wa utandawazi,teknolojia imekuwa,Nchi inawasomi wengi,bado tunafeli,alafafu tunazungumzia kukua kiuchumi?

Unawezaje kukua kiuchumi kwa kutaka kugawana faida na watu wengine,tena faida inayotokana na kiungo muhimu kama cha bandari?

kama tunafanya hivyo kwa faida ya Taifa,basi tungeanza na zile sekta ambazo mpaka sasa hazijafanya vizuri kama nishati,secta ya nishati mpaka leo bado ni kichwa cha mwendawazimu,Tutafute wabia kwaajili ya TANESCO,ili umeme uzalishwe kwa wingi na kwa uhakika,kukatika katika kuwe historia,

Tutafute wawekezaji waje wasimamie madini yetu ili yasitoroshwe,na waendeleze na kufanya utafiti wa maeneo mapya yaenye madini na nishati nyengine kama gesi,makaa ya mawe nk..,hizi ndizo sehemu naoana kama taifa tumeshindwa kabisa kusimamia.

Na hatuoni kama tutaweza kuyasimamia ipasavyo maeneo haya,lakini sio bandari,sehemu ambayo inahitaji tu uwekezaji mdogo ili ulete tija kubwa, napo tushindwe? Labda kama tunatania hatutaki kwenda mbele,kwasababu sidhani kama kuna nchi iliyoendelea kwa kutafuata wabia katika sekta zake muhimu,sijui lazima tujitafakari kama Nchi,tunania thabiti au tunatawaliwa na hisia na mihemuko pamoja na tamaa.
 
Back
Top Bottom