Kwanini waziri wa fedha asiombwe kujiuzuru, kama...

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363




Atashindwa kuwasaka, kuwakamata na kuwafikisha kwenye mikono ya sheria wale wote wenye kuhusika na kashfa hii inayoitia aibu Taifa akiwemo Rais wa Nchi.

Shilingi milioni 600 zimetafunwa halafu tukae tukimchekea Waziri wa Fedha hata pale anaposhindwa kuwasaka, kuwakamata na kuwafikisha kwenye mikono ya sheria wahusika wa uhalifu huu. Itakuwa ni jambo la fedheha sana.

Tayari Sweden na Finland wameshasimamisha kutoa fedha zaidi kusaidia programu hii ya maboresho kwa tawala za mikoa ikiwemo halmashauri zetu. Wana sababu za kufanya hivyo na

zaidi pale sisi wenyewe tunaoonyesha kuwachekea wahalifu wetu. Ambao kimsingi ni wezi na wabadhirifu wa fedha za umma. Fedha za wananchi.

Tunaambiwa maafisa wetru wametumia fedha pia kununua magari ya kifahari. Kulipana kwa viwango vya ajabu posho za vikao na marupurupu mengine.(P.T)

Na wizi huu wanaufanya huku wakijua kuwa Wananchi wa kawaida waliolengwa kwa misaada hiyo ndio wenye kuathirika zaidi. Ni ubinafsi wa hali ya juu.

Na tarehe 5 Desemba Waziri Kivuli wa Fedha, Mh. Zitto Kabwe amealikwa kwenye kongamano la jubilei ya Miaka 50 ya Ushirikiano wa Sweden na Tanzania. Naye, hata kama yuko bize na ' Vita'

vya ndani ya chama chake ni lazima awe na majibu kwa washirika wetu hawa wa Kimaendeleo juu ya hatua zinazochukuliwa katika kushughulikia ubadhirifu huu wenye kuwakatisha tamaa hata Washirika wetu wa Maendeleo.
Maggid Mjengwa.
Iringa.
0754 678 252

chanzo.
Kwanini Waziri Wa Fedha Asiombwe Kujiuzuru, kama...



 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…