Kwanini wenzetu Sweden wanapenda kulipa kodi?

Action and Reaction are Equal and Opposite...

Kama unapata benefits za kutosha hata kama haupendi huwezi kulaumu mchango wako wa kodi, ila ndio kama hivyo benefits mpaka uambiwe na kuwekwa shule kwamba hiki na kile ndio kimefanyika (nadharia kuliko uhalisia) lazima uone tabu ku-part with your hard earned cash...
 
Sweden ni mali ya wa Sweden wote, bongo ni mali ya mtu binafsi
 
Hacha kupotosha chief, issue ya kodi aina mausiano yoyte na umri wa nchi,

Hapa tunachotakiwa kusema ni mifumo mibovu ya uendeshaji nchi, na siyo swala nchi gani kongwe na nyingine syo kongwe,
Nadhani ukifikiri kwa makini utaelewa maana ya MUDA.
Taifa lina karne 15 za kujijenga na kutengeneza misingi imara ya kijamii, kiutamaduni, kisiasa, kiuchumi, (ikiwemo mifumo ya kodi)nk.
Kabla sisi hatujapata uhuru wao tayari walikuwa:
Walishajitawala kwa miaka. 1500;
Wamefuta ujinga 100%
Wamesambaza maji 100%
Umeme 100%
Huduma za afya.
Reli Barabara Bandari viwanja vya ndege100%
Wanamaendeleo makubwa ya sayansi na teknolojia na mapinduzi ya viwanda.
Uchumi mkubwa (wanauza magari ya SCANIA dunia nzima). Aidha makampuni yao makubwa yenye mamia ya miaka yametapakaa Dunia nzima kupitia mifumo ya hisa na hivo mirija hiyo inafyonza utajiri toka duniaani kote.
Kifupi walikuwa wameweka miundo ya kijamii na kiuchumi ambayo multiplier effect yake ni kutengeneza mifumo ya ajira na kujiajiri na kuimarisha biashara, kutoa mikopo na ruzuku hifadhi ya jamii na mafao kukosa ajira kwa wananchi.
Hizi ndio sababu wameweza kukusanya kodi kubwa sana.
Kwa mfano Sweden wana wigo mpana ukusanyaji kodi na wakusanya 43 ya ya GDP, ukija kwenye kodi ya mapato wanachukua mpaka 57% ya mshahara.. yaani kama unapokea milioni wanachukua takriban laki tano na na sabini. Wakati makusanyo yao ni makubwa bado hawahitaji kuongeza mashule..mahospitali.. mabarabara mareli viwanja vya ndege mabandari kufua umeme au chochote.
Je Umejiuliza hayo mapato ya kodi yanaenda wapi sasa!?
Bila shaka ni kutoa huduma bora na zingine bure kwa wananchi na kutoa misaada kwa mataifa masikini kama sisi.
 
china,india, north korea hazina biblia wala msaafu nahc unajua kinachotokea
 
UTAPATA wapi huduma hizo Bure kama Matumizi ya Serikali ni Asilimia 75 ya Makusanyo ya Kodi? Magari ya Viongozi ya Kifahari toka ya Chama Tawala Wakurugenzi Ma DC,Rc,Makatibu Wakuu Mawaziri n.k?Mishahara ya Wabunge Kufuru
 
Tanzania wakati wa Nyerere elimu ilikuwa bure na matibabu bure na ajira bwerere tele serikalini na watu walikuwa wagumu kulipa kodi!! Hayo ya sweden tulishapita huko watanzania kwenye kodi vichwa ngumu
Mpaka Polepole atakapoacha kutambia Vieitee za viongozi wa CCM ndo tutaanza kulipa kodi kwa hiari. Kama tunalipa kodi halafu mtu anatumia kodi yako kukusimanga, tutaendelea kuburuzana mpaka tunaingia kaburini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…