Kwanini Yanga wanashangilia sare

Kwanini Yanga wanashangilia sare

HPAUL

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2011
Posts
410
Reaction score
567
Mjini hakukaliki, Yanga tangu wamepata sare na Simba wameshangilia sana matokeo hayo kama vile ambavyo Simba ingeshangilia kupata sare na Real Madrid.

Je, ni kweli kuwa kiwango cha Yanga kwa sasa kimeporomoka sana kiasi cha kuona sare na Simba ni miujiza na ushindi mkubwa.

Takwimu zinaonyesha Yanga kwa zaidi ya mwaka moja na nusu hawajafanikiwa kuifunga Simba.
 
Hiyo ni kawaida mzee sio bongo tu hata ulaya haya mambo yapo na yanasababishwa na hizo timu kipindi zinakutana zipo katika hali gain, juzi tu Chelsea kashangilia sare mbele ya liver
 
Wewe una mambo ya ajabu hujui kama Chelsea alimpiga liver kwake au umesahau?
 
Mjini hakukaliki, Yanga tangu wamepata sare na Simba wameshangilia sana matokeo hayo kama vile ambavyo Simba ingeshangilia kupata sare na Real Madrid. Je ni kweli kuwa kiwango cha Yanga kwa sasa kimeporomoka sana kiasi cha kuona sare na Simba ni miujiza na ushindi mkubwa. Takwimu zinaonyesha Yanga kwa zaidi ya mwaka moja na nusu hawajafanikiwa kuifunga Simba.
Kwanini wewe aushangilii??
 
Kumbuka mwaka 2014/15 kama sijakosea wakati huo Yanga ilikuwa juu sana kwa kiwango cha uchezaji kuliko Simba. Simba ilitoka sare na Yanga tena golini akiwa Manyika junior. Simba hawakuamini kilichotokea wakishangilia zaidi miezi 2. Hii inatokea pale ambapo hizi timu mbili, moja iko juu na nyingine iko underdog. Kwa hiyo usishangae sana ndugu.
 
Hiyo ni kawaida mzee sio bongo tu hata ulaya haya mambo yapo na yanasababishwa na hizo timu kipindi zinakutana zipo katika hali gain, juzi tu Chelsea kashangilia sare mbele ya liver
Acha uongo wewe,

Chelsea alikua anaongoza 1-0 Liver wakasawazisha dakika za mwishoni 1-1 sasa hapo kwa akili ya kawaida tu,ni nani anayepaswa kufurahia droo?

Liver ndio waliyo ifurahia droo na waliitafuta droo juzi tu hapa dhidi ya Napoli ila wakapigwa 1-0 dakika za mwishoni.
 
Hiyo ni kawaida mzee sio bongo tu hata ulaya haya mambo yapo na yanasababishwa na hizo timu kipindi zinakutana zipo katika hali gain, juzi tu Chelsea kashangilia sare mbele ya liver
Huoni liver ndo walisherehekea kupata droo..
 
chersea ndio alisheherehekea ndio maana kabla ya mechi ni washabiki wa liver pekee walikuwa wanauwezo wa kuongelea ile mechi ila baada ya mpira kuisha washabiki wa blues wakawa wanawazomea washabiki wa liver
 
sasa anaachaje kusherekea sare ili hali inampa point 1 huku akiwa juu ya simba

anaachaje kushangilia ikiwa inamfanya kutopoteza mchezo mpaka sasa.

kikosi cha billioni kupambana na kikosi cha robo billion kwa nini usishangilie
 
Mjadala umefungwa
 
Yanga inaangalia nafasi kwenye msimamo wa ligi. Hatuhitaji mbwembwe zaidi ya kurudisha Kombe nyumbani kwake lilikozoea
 
Mjini hakukaliki, Yanga tangu wamepata sare na Simba wameshangilia sana matokeo hayo kama vile ambavyo Simba ingeshangilia kupata sare na Real Madrid. Je ni kweli kuwa kiwango cha Yanga kwa sasa kimeporomoka sana kiasi cha kuona sare na Simba ni miujiza na ushindi mkubwa. Takwimu zinaonyesha Yanga kwa zaidi ya mwaka moja na nusu hawajafanikiwa kuifunga Simba.
Kimsingi Yanga inashangilia kufanikiwa kwa mpango mkakati wa kukabiliana na kikosi cha Simba katika hali ya sasa wala sio sare. Ukipambana na adui (mpinzani)yako huna budi kujua nguvu zake na udhaifu wake dhidi ya nguvu zako na udhaifu wako. Halafu unatengeneza mpango wa kukabiliana nae ama ushinde au usiposhinda asipate fursa ya kukushinda. Kwa Yanga hilo limefanikiwa na limepunguza shinikizo linalotokana na kushindwa. Unapowadharau unakuwa hujaelewa kilichotokea. Adui kaachwa na shinikizo lake la kushindwa na pia hajui kitakachotokea baadae. Na kwa kuwa alishjipangia matokeo yake na ikawa sivyo anaumia zaidi. Ndivyo ilivyo kwa kila jambo. Ila sio kila MTU anaweza kuona au kufanya hivyo.
 
Mjini hakukaliki, Yanga tangu wamepata sare na Simba wameshangilia sana matokeo hayo kama vile ambavyo Simba ingeshangilia kupata sare na Real Madrid. Je ni kweli kuwa kiwango cha Yanga kwa sasa kimeporomoka sana kiasi cha kuona sare na Simba ni miujiza na ushindi mkubwa. Takwimu zinaonyesha Yanga kwa zaidi ya mwaka moja na nusu hawajafanikiwa kuifunga Simba.
Mashabiki mbumbumbu kama wewe hata Comoro hawapo.
 
Mjini hakukaliki, Yanga tangu wamepata sare na Simba wameshangilia sana matokeo hayo kama vile ambavyo Simba ingeshangilia kupata sare na Real Madrid. Je ni kweli kuwa kiwango cha Yanga kwa sasa kimeporomoka sana kiasi cha kuona sare na Simba ni miujiza na ushindi mkubwa. Takwimu zinaonyesha Yanga kwa zaidi ya mwaka moja na nusu hawajafanikiwa kuifunga Simba.
Yawezekana ukawa sahihi ila kwa kukukumbusha tu, Yanga hadi sasa hawajapoteza mchezo hata mmoja, pili; Sare in alama 1, hivyo, imeongeza alama 1 ktk alama za Yanga, tatu, japo ligi ipo mwanzoni, Yanga bado ipo juu ya Simba. Sielewi kwamba ulitaka walie!? Mtani bwana una vituko [emoji38][emoji38]
 
Mjini hakukaliki, Yanga tangu wamepata sare na Simba wameshangilia sana matokeo hayo kama vile ambavyo Simba ingeshangilia kupata sare na Real Madrid. Je ni kweli kuwa kiwango cha Yanga kwa sasa kimeporomoka sana kiasi cha kuona sare na Simba ni miujiza na ushindi mkubwa. Takwimu zinaonyesha Yanga kwa zaidi ya mwaka moja na nusu hawajafanikiwa kuifunga Simba.
Ni kweli kiwango cha Ndala kimeporomoka kwa kasi ya 4G.
 
Back
Top Bottom