Kwanini Zambia Wameweza Kuuangusha ‘ mbuyu’ – Ivory Coast?

maggid

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2006
Posts
1,084
Reaction score
1,246
Ndugu zangu,

Ukitaka kuukata na kuuangusha mbuyu usianze kufikiria unene wake. Jana usiku jirani zetu Zambia wameafanya maajabu ya soka. Vijana wa Chipolopolo wamatwaa ubingwa wa Afrika kwa kuwafunga Ivory Coast.

Ndio, Zambia jana wametufanya tujisikie, kuwa; " We are all Zambians". Kwamba sote ni Wazambia.


Siri ya ushindi wa Zambia?



Ni Uzambia. Ni utaifa. Ni uzalendo. Tuliwaona vijana wa Chipolopolo wanaojituma uwanjani. Vijana waliokuwa tayari kufia uwanjani, Vijana kama akina Kampamba, Mulenga, Sunzu, Nkausu, Chansa na wengineo.

Na katika maisha, ili mwanadamu afanikiwe unahitaji kuwa na ' K' tatu; Kujitambua, Kujiamini na Kuthubutu.

Vijana wa Chipolopolo wamejitambua. Wameijua historia yao. Wamejua walikotoka. Wamejua, kuwa kuna baba zao, mwaka 1993 walikuwa njiani kwenda Senegal kucheza mechi muhimu kufuzu kutafuta tiketi ya kucheza Kombe La Dunia. Usafiri ulikuwa mgumu. Walipanda ndege ya jeshi. Ndege ilianguka pwani ya Gabon, wachezaji wote 18 walipoteza maisha. Walikufa kwa ajili ya nchi yao.


Ndio maana jana, kwa kuitambua historia hiyo. Wazambia wale waliingia uwanjani wakiwa tayari kufia uwanjani kwa ajili ya nchi yao. Tulimwona beki Joseph Mussonda akiumia vibaya. Alijikaza kuendelea. Ikaonekana haiwezekani kabisa. Akatolewa nje. Alitokwa na machozi kwa muda mwingi. Si kwa maumivu ya mguu tu, ni kwa kuona uchungu wa kukosa kuwa uwanjani kuipigania nchi yake. Huo ni moyo mkubwa wa uzalendo. Wazambia wale hawakuwa wakifikiria posho zao, bali taifa lao. Na hakuna ahadi yoyote ya fedha waliyopewa kabla ya mechi ya jana.


Ndio, Wazambia wale walionyesha kujiamini sana. Walicheza mpira wao. Walikuwa focused muda wote. Hawakujali majina makubwa kama ya akina Drogba, Kolo Toure, Yahya Toure, Koite, Gervinjo, Gosso Gosso na mengineyo. Hawakujali kama walicheza na nyota wanaovichezea vilabu vikubwa huko Ulaya. Chipolopolo walicheza mchezo wao. Mwanzo hadi mwisho. Hata pale Ivory Coast walipokuwa wakijaribu kubadilisha mbinu na hata kubadilisha nafasi za wachezaji uwanjani, bado Zambia waliendelea kucheza mpira wao.

Kuna mengi ya kujifunza kutoka kwa jirani zetu wa Zambia. Nitaendelea na uchambuzi wangu…

Maggid Mjengwa,
Iringa.
Jumatatu, Februari 13, 2012
Mjengwa Blog::Habari,Picha,Matangazo
 
Misuse of space!! Do you think this has anything to do with "Jukwaa la Siasa" at all?? I dont feel Zambian just because they are champions. Would I call myself Ivorian if they won?? No, I would not!!!

Take your post to an appropriate place!!
 
Msaada wetu kwa wazambia huu hapa!!

 
Majjid,
Umenena vema na umetoa mtazamo mzuri, ila thread umeiweka jukwaa la Siasa badala ya sehemu yake husika.
Ndio, yapo mengi sana ya kujifunza toka Zambia. Ni vigumu sana kwa Tanzania kupata mafanikio kama ya hao majirani zetu, kwani Siasa na ubabaishaji ndio vinavyotawala na kuendesha soka.
 
Ama kweli, wazambia wathubutu, wameweza na wanasongambele, Mungu ibariki Zambia, Mungu ibariki Afrika. Tanzania bado tuko kwenye michakato, na tayari raisi wa TFF ameshaunda task force na negotiation team mara tu baada ya mchakato huu nadhani tutashiriki world cup,ila mpaka huumchakato uishe, na tufanye upembuzi yakinifu, hapo tutakuwa fiti
 
Nasi Tujiandae kisayansi. Mpira hauchezwi kwa kaulimbiu za kisiasa. Baada ya ajali iliyopoteza maisha ya timu nzima ya taifa ya zambia,nchi hiyo ilianza kuwekeza , projection yao wakijua kabisa miaka hii ndio itakuwa mavuna,na kweli tumeona! Vyama vyetu vya michezo bado vinawababaishaji.wizarani wapo.tff napo mi sisemi ila maandalizi yao ya zimamoto wote twayaona. Sasa hawa wababaishaji wanapokuwepo kwenye mfumo huu mzima ndio kwa kiasi kikubwa wanakuwa kansa inayotafuna ari , uzalendo wa wachezaji na maendeleo ya michezo yetu kwa ujumla. Viongozi wasio na vision wasipewe nafasi, Wezi na wasio wazalendo tupa pembeni na mwisho tusilazimishe uzalendo utoke tu kwa wachezaji, uzalendo uanzie kwa viongozi wa ngazi zote na tafsiri yake tuipate mwishoni kwa wachezaji. Wachezaji wanaodhulumiwa stahili zao hawawezi kuwa na uzalendo hata kdogo.
 
through the triumph of Zambia i have come to the conclusion that for one to succeed he7she needs to be respector of principles and not be the respector of names.
 
Angalau kombe limekuja sub saharani Africa
 
mungu awabariki siha njema chipolopolo na tuwaombee safari njema kurudi nyumbani kwao Zambia.
AMEN
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…