Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,184
Mwanasiasa machachari, kijana na Mbunge wa upinzani Zitto Kabwe amekuwa akihimiza misimamo yenye migongano mingi kimasilahi na kuwapa upepo usiyo wa lazima mahasimu wake kisiasa kumvika joho la uchu wa madaraka ya kitaifa na haya ni baadhi tu ya maeneo ambayo yanamtia hatiani Mheshimiwa huyu:-
1) KWENYE kasheshe ya Buzwagi ambayo ilimweka kwenye chati ya siasa za nchi hii Bungeni alipinga vikali mikataba ya madini akidai ni ya kinyonyaji lakini JK kwa kushawishiwa na BARRICK GOLD alipompa ugali wa kula kwa kuwa mjumbe wa kamati ya Raisi kuchunguza na kushauri kuboresha mikataba ya madini Zitto Kabwe sasa hana matatizo na sheria na mikataba ya madini maana tumbo lake limeshibishwa vilivyo na BARRICK GOLD.
2) KWENYE ulaji wake alipokuwa Mwenyekitebe cha POC alikuwa mstari wa mbele kuhoji migongano ya kimasilahi kwa wabunge kuteuliwa nafasi za kiutendaji ndani ya serikali wanayoisimamia na hata alidiriki kusema hizo ni hongo za kuwaziba midomo wabunge wapelee kuisimamia serikali Bungeni lakini kuteuliwa kwake na JK akiwa mbunge kufanya kazi za kiutendaji kama kuchunguza namna ya kuboresha sheria na mikataba ya madini hakuona kuna migongano ya kimasilahi kwa sababu moja tu tumbo lake lilindwa vilivyo na BARRICK GOLD .
3) KWENYE ufisadi wa DOWANS pale TANESCO; akiwa mwenyekitebe cha POC, aliunga mkono walipwe hata kama hawakufanya kazi na hakuona uhaja ya wale waliotufikisha hatua ile kuaadibishwa! Mashinikizo tajwa ya watendaji wengi serikalini na baadhi ya wabunge kama Zitto yalitokana na kuahidiwa kumegewa kipande cha mkate na DOWANS na ndiyo maana walikuwa wakitetea walipwe.
4) KWENYE ufadhili wa BARRICK GOLD katika miradi mingi kwenye jimbo lake hususani ya elimu, Zitto Kabwe haoni kuna migongano ya kimasilahi kupokea hongo kutoka kwa wawekezaji ambao mikataba yao haramu alishiriki kuichunguza katika kamati teule ya Raisi na kutotoa ushauri wowote ule wenye masilahi kitaifa zaidi ya kusisitiza wahusika wana mikataba ambayo lazima iheshimiwe bila ya kuona mikataba yenyewe ni batili na hivyo haipaswi kuheshimiwa mbali ya kuleta ubaguzi ndani ya sekta ya madini
5) KWENYE wadhifa wake wa Unaibu katibu Mkuu wa CDM na ujumbe wa kamati kuu ya CDM haoni amejirundikia madaraka wakati yeye pia ni mbunge lakini yuko mstari wa mbele kudai Raisi apunguziwe madaraka kwenye mapendekezo ya katiba batili ya marekebisho! Hajawahi kuhoji uhalali wa Bunge kupitisha sheria ya marekebisho ya katiba ambayo inakinzana na utaratibu ulioanishwa na katiba iliyopo na hivyo kufanya zoezi zima kuwa ni ukiukwaji wa katiba iliyopo!
6) KWENYE wadhifa wake wa Unaibu katibu Mkuu wa CDM na ujumbe wa kamati kuu ya CDM haoni ana migongano ya kimasilahi pale anapohoji CDM kutopeleka mizania yake kwa CAG kwa takribani kipindi cha miaka mitatu huku ni mshiriki wa vikao vyote vya juu vya CDM ambako angeliweza kushauri makosa hayo kama yapo yarekebishwe.
7) KWENYE wadhifa wake wa Unaibu katibu Mkuu wa CDM na ujumbe wa kamati kuu ya CDM hasikii harufu kali ya wizi na ubadhirifu mkubwa unaoendelea ndani ya CDM wa fedha za wafadhili na za ruzuku kutoka serikalini na hajawahi hata kukemea zaidi ya kujitenga na wenzake kwa sababu tu hawamuungi mkono katika azma zake za kugombea Uraisi mwaka 2015.
8) KWENYE wadhifa wake wa sasa wa mwenyekitebe cha PAC amekuwa akihoji sana mishahara ya Raisi na Waziri Mkuu bila ya kutuelezea watanzania kwa sababu zipi bungeni hajawahi kupeleka muswada binafsi wa kutengua mishahara hiyo ikiwemo ya wabunge ambayo kila mwezi hupeperushiwa kwenye akaunti yake bila ya yeye binafsi kukerwa na uporaji huo wa wazi wa mali za umma.
9) AMA Vyeo ambavyo Zitto Kabwe amekuwa akivisaka kwa udi na uvumba ni Uraisi na uenyekiti wa CDM na migogoro aliyonayo na wenzie ndani ya CDM ni pale anapobaini wamekuwa kikwazo cha yeye binafsi kufanikisha azma zake za kukamata dola ..
10) AMA Zitto Kabwe aliahidi kuwa mbunge kwa vipindi viwili ambavyo vinafikia ukomo mwaka 2015 lakini kampeni za tamaa za mzee fisi za kuendelea kuwa mbunge kama uraisi utashindikana nazo anazichochea bila kuweka wazi mabadiliko ya ahadi zake yanachochewa na nini..........
KWA HULKA NA SILIKA kama hizi hivi mahasimu wake wa kisiasa ndani na nje ya CDM wanakosea kumwona ana uchu wa madaraka ya kukamata dola tu?