Kwann watu wanaidharau degree ya Open University?

Nimebahatika kufanya kazi na watu zaidi ya watatu waliosoma OUT, Kiukweli pale hakuna Elimu bali ni mkakati tu wa kuwapatia digrii kwa wasio kuwa nazo ila kimsingi kichwani ni EMPTY (Too shallow).
Mimi nadhan kwa bachelor ule mfumo haufai labda kwa MA kidogo maana mtu anakua matured enough academically
 
Wadau ni kwann mhitimu wa degree kutoka OUT anadharaulika na kuonekana kama degree yake haipo sawa kama degree nyingine kutoka vyuo vingine?
siyo tuu Openi University ,Mbona hata zile MBA za evening za Mzumbe Dar es salaam Campas nazo zilikuwa zinadharauliwa sana,walikuwa wanaziita za kichina. Achana na watu.dunia ya sasa watu wanaangalia uwezo wa msomi mwenyewe na siyo chuo alichosoma
 
umefanya na watu watatu una reflect kqamba out product zote ziko hivyo?
siwatetei but sikuiz chuo doesnt matter.. ni jitihada za msomi mwenyewe.
as i know OUT wanasoma watu walioko kazini ninwachache sana wanaotoka advance na kuenda out moja kwa moja.
sasa mtu ambae anaongeza elimu ni tofauti na anaeanza.
 
Wadau ni kwann mhitimu wa degree kutoka OUT anadharaulika na kuonekana kama degree yake haipo sawa kama degree nyingine kutoka vyuo vingine?
Ukiwa umesoma OUT harafu usome uzi kama huu
Unaweza kujihisi kuugua kabsa
 
A person studied in college A and got a job in college B. Then studied at OUT.

The person's comparison of education at college B and at OUT: real education is at OUT. At college B, the students are lazy, disinterested in learning, 'wanakremisha madesa yaliyopitwa na wakati', pretending that they are learning. Kule OUT ni shule mtindo mmoja. That was the person's assessment.
 
Wadau ni kwann mhitimu wa degree kutoka OUT anadharaulika na kuonekana kama degree yake haipo sawa kama degree nyingine kutoka vyuo vingine?
Pana shule ngumu sana pale ndugu, anayedharau atakuwa hajapitia pale bila shaka. Na hizi dharau hazijaanzia OUT tu, walianza kuwananga Mzumbe University, kwamba degree zao feki. Nadhani soko pia linaamua pia aina ya degree na inakopatikana.
 
Aisee Mwanza maeneo ya Mkolani kuna Tawi linajengwa la OUT ni bonge la mjengo
Hatuangaliii majengo kikubwa utoaji wa elimu kiukweli out ni chuo maalumu kwa ajiri ya waajiriwa na ndio maana now wana 50%reduction fee kwa wanao soma education lakin uwe kwanza mwajiliwa na kada yako ni ualimu kiukweli sasa wameanza kwenda na wakati ni chuo kizuri sana usikiseme vibaya kua wahitimu wake hawapati ajira kwani wanao ongoza mtaani kwa kutokupata ajira wanatoka tu open tuwe makini na elimu za watu
 
Aisee Mwanza maeneo ya Mkolani kuna Tawi linajengwa la OUT ni bonge la mjengo
Acha fix Mwamba!! Mkolani ipi, Vijengo Kama Hizi Private candidates centre!!! Au kile kighorofa Cha pembeni ndio kimekuchangaya!! Pale Hakuna Ujenzi wowote mkuu!!! Lile jengo ni la mtu Binafsi tu
 
KUna maeneo umenena vyema ila umepotosha sana kusema kuwa Chuo Kikuu Huria yeyote anasoma bila kujali kama alifaulu ama hapana huko nyuma, hii si kweli, Chuo Kikuu Huria ni Chuo Kikuu kama vilivyo Vyuo Vikuu vingine, huwez kujiunga na ngazi yoyote ya Elimu bila kuwa sifa stahiki kamam zilivyowekwa na TCU au NACTE
 
Naona wengi tunakoment kishabiki, kwa sababu bado naona watanzania tuna ule ugonjwa wa kuona chuo ulichosoma wewe ndio bora kuliko vyuo vingine, hili janga kamwe haliwezi isha kama hatutofikiri kitaaluma zaidi!!!

1.Binafsi nmesoma mifumo yote miwili, Conventional (Kukaa darasani kama vilivyo vyuo vingi) na Distance Learning (wanaotumia OUT na vyuo vingi sasa Duniani). Nmeona changamoto za mifumo yote, lakini kote unapata content ile ile , ila katika conventional system kule tunakua kama kuku wa kisasa, tunategemea kulishwa kila kitu na wahadhiri, ila kwa Distance Learning pamoja na kuwa unapewa materials zote (tena nahisi kuliko kwenye conventional system) ila issue ni kuwa kwa kuna interaction ndogo sana ya face to face na wahadhiri hivyo ni lazima ujipinde zaidi wewe binafsi katika usomaji ili uweze kutoboa.

2. Ubora wa Graduate yeyote hauwi determined na Chuo alichosoma, bali unakua determined na personal efforts, nmesoma katika mifumo yote miwili na nmeliona hili sana, so, tusidanganyane kuwa Chuo A kiko bora zaid kuliko Vyuo hivi na vile, nope, ni juhudi binafsi za mtu ndio zinamfanya awe bora, sasa wewe ukikutana na huyo alie bora utamuuliza kasoma chuo gani akikutajia una-conclude kuwa chuo chao ni the best, hivyo hivyo mtu mwingine akikutana na graduate mzembe mzembe kutoka chuo kile kile ata-conclude kuwa chuo hicho ni hovyo, so tuache kasumba hizo tuangalie performance ya mtu na kumpima yeye mwenyewe na sio kuhukumu chuo either negatively au positively!!
Tuelimike
 
Acha fix Mwamba!! Mkolani ipi, Vijengo Kama Hizi Private candidates centre!!! Au kile kighorofa Cha pembeni ndio kimekuchangaya!! Pale Hakuna Ujenzi wowote mkuu!!! Lile jengo ni la mtu Binafsi tu
Kwenye ofisi za NiDA upande wa pili kulia wanajenga nyumba ya mtu pale?? Mkuu pita usome vizuri na bango lipo limeandikwa kwa herufi kubwa
 
Wewe ndio hukusoma vizuri niliyoyaandika. Wapi nimepotosha?
 
 
Nimejaribu sana kuwaelezea hapa JF kuwa Distance Learning kama OUT inaonyesha ukomavu wa akili.
Lakini hapa tunaongea na vitoto vya sekondari , hawawezi kukuelewa
Wakati dunia nzima mpaka vyuo vikubwa duniani vinaongeza kwa kasi mfumo wa Online course na qualification zina viwango sawa na onsite learning.
Na COVID kwa nchi nyingi ndio imeonyesha mtindo huu wa elimu unawezekana.
 
Na baada ya Janga hili la COVID-19 tutarajie kuona vyuo vingi Duniani vikitumia mfumo wa Distance Learning, wenzetu East Africa hii hiikuna vyuo sa hivi wana mifumo bora kbs ya Distance Learning, ngoja sie tuendelee kushangaa shangaa na kukariri elimu ni haid umuone mwalimu kasimama mbele lecture theater anapiga mikwara yake basi!!
 
Nimesoma out ngazi ya graduate program, asikwambie mtu elimu ya pale Ni ngumu balaa kuliko hata nilivyokuwa nasoma under graduate Tena direct entry kutoka form six. Mnaosema pale rahisi nendeni mkasome pale japo short course ya miezi 3 au 6 uone Moto wake.
 

Ni kweli kuna tofauti kubwa ya anaesoma Mathematics kwa Distance Learning na kwa Face to face.
Yaani Mtu anasoma Concept bila kufundishwa mpaka anaelewa, bila shaka ni ukomavu wa akili.
 
Ni kweli kuna tofauti kubwa ya anaesoma Mathematics kwa Distance Learning na kwa Face to face.
Yaani Mtu anasoma Concept bila kufundishwa mpaka anaelewa, bila shaka ni ukomavu wa akili.
uko sahihi kabisa, watu wengi wamezoea kumezeshwa tu ndio shida hapo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…