Ni muhimu sana kupata KATIBA MPYA kabla ya kuingia kwenye uchaguzi ujao wa 2015.
Tukipata katiba mpya tutaweza kupata TUME HURU YA UCHAGUZI, TAKUKURU HURU na UCHAGUZI HURU KUANZIA 2015 na mambo haya ya uchakachuwaji yatapotea kabisa. Pia chini ya Katiba Mpya tutaweza kumuadabisha hata Rais akienda kinyume na Katiba. Kwa Katiba ya sasa Rais aliye madarakani na wale wastaafu hawawezi kushitakiwa hata kama anafanya/walifanya udikiteta wakiwa madakani
Tusije tukajidanganya kufanya uchaguzi bila kuwa na Tume huru ya Uchaguzi; kwani CCM na vibaraka wao Tume ya sasa ya Uchaguzi (NEC) wataendelea kuchakachuwa kura.
Wenzetu wakenya wamepata KATIBA MPYA, TUME HURU YA UCHAGUZI NA TAASISI HURU YA KUZUIA RUSHWA na mambo yao yanaenda vizuri kwa sasa. Mafisadi wote wanapelekwa mahakamani chini ya Katiba Mpya bila kujali cheo cha mtu.
Swala hili la KATIBA MPYA, TUME HURU YA UCAGUZI na TAKUKURU HURU ni kwa faida ya kila mtanzania na ni lazima mtanzania yeyote mwenye uchungu na raslimali za nchi yake, anayeweka maslahi ya Taifa mbele lazima avipiganie hivyo. Naomba vyama vya SIASA vya Upinzani na ASASI ZA KIRAIA vituongoze katika hili. Kama wakitaka kuandamana "We are more than ready to do that" (Tupo zaidi ya tayari kuandamana kwa ajili ya Katiba mpya)
CCM hawako tayari kuandaa mkutano wa Katiba Mpya na Tume huru ya Uchaguzi inabidi wananchi tuwashinikize kwani wanataka waendelee kuchukuwa raslimali za nchi kwa manufaa yao. Nadhani unakumbuka walivyofanya EPA, RICHMOND, BUZWAGI, MEREMETA, IPTL na mikataba mingine mingi (listi ni ndefu).
Watanzania tuamke tuwe tayari bila kujali itikadi ya chama kuyapiganiya hayo kwani ni kwa maslahi ya watanzania wote na KIZAZI KIJACHO!!!!!!!!