Kweli baadhi ya wanawake hawaridhiki

ndonger

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2018
Posts
894
Reaction score
1,635
Ni hivi, huyu bibie kama miaka miwil nyuma hivi nilikua sijapata kazi ya maana, yaani ilikua nafanya kazi hii narukia hii, au nafanya kazi mbili kwa wakati mmoja.

Kama mnavyojua kazi na agencies, kama kazi zipo warehouse basi mnaenda kama hamna mnatulia. Basi huo ndiyo ulikua mtindo so nikawa mara nyingi nakua break so tunakua na muda fulani wa kupumzika nayeye.

Ikawa ni maneno ya hapa na pale kwamba hamna stable income na mama yake nadhan alikua anachangia kumpamp.

Sasa nina kama miez 7 hivi nina kazi nyingne ambayo mkataba unanibana kwelkweli. Napiga kazi 12hrs na kama mnavyojua watu weupe ni kazi kazi hakuna kutegea.

Ni kampun kubwa na wanalipa vizuri so sina shida kwenye income ila ndo kazi yenyewe ni u anapigika kwelikweli yaani siku ya kupumzika ni unalala tu siku mbili mfululizo..

Mahitaj natoa kama kawaida. Yeye pia anafanya kaz ila ili nisionekane ngoz nyeus kinyonge so mahitaj meng nacover mimi.

Ni hivi hizi ngozi nyeupe zna stereo types na beliefs nying sana kuhusu ngoz nyeus so kama hu provide bas ni majungu,wana majungu hawa balaa. Basi najitahid sana.

Tatzo lilopo sasa nalaumiwa
1. Sina muda naye

2. Nalala tuu muda wote nikiwa home

3. Simsaidii kazi za home

4. Muda wote niko na simu. Kiukweli muda mwing huwa niko na simu maana nikiwa job simu huwa hatutumii so nikiwa break ndo muda wangu huu na mara nying niko youtube, instagram au facebook kuchek matukio yanayoendelea nyumban bongo, sababu sio siri namiss bongo kinoma.

Sasa wadau, hivi kuna mode yoyote ya jinsi ya kuish na wanawake bila kelele.

Yaani nikawa na amani au ndiyo haiwezekani kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…