Kweli hapa kampuni za simu mnawaibia wa Tz bila huruma..Gvnt Kimyaaa

Joined
Jan 27, 2013
Posts
36
Reaction score
7
Hisabati rahisi ya haraka ya kujumlisha na kutoa: Eti Vodacom wanakusanya shilingi ngapi kwa siku ktk shindano lao la MAHELA ambapo VODA watatoa ZAWADI za Tsh mil 400 tu hadi mwisho? Kila SMS ni 350. watu wanatuma SMS nyingi hadi wanasahau kubajeti fedha zao..Rafiki yangu kashatoa sh 50,000 ktk mshahara wake na kucheza huo mchezo. sijui ni wangapi wametoa mishahara yao kwa hilo. Voda wanatuambia kuwa wameamua kutoa zawadi ya 400m. Uongo, hizo ni 350 zenu. Nafikiri hii ni hatari ktk uchumi wetu wa kimaskini hapa Tz.. Huu ni ufisadi mwengine na kushusha thamani ya sh. na najua waziri wa fedha anajua hili vizuri na analikalia kimya; haiwezakani kampuni za simu ziachwe zikusanye mabilioni ya wa Tz bila sababu za kiuchumi...Kiuchumi, mtu anapotumia sh. 350 bila sababu za kiuchumi ni hasara kiuchumi..hata hamnielewi..tunaibiwa jamaniii...Kwa nini Kenya walipiga marufuku michezo hii ya simu?
 
...Hivi Kuna Watu Bado Wanacheza Hizi Bahati Nasibu za Kitapeli za Haya Makampuni Ya Simu za Kiganjani?? Kwanza Pole zao na Kisha Tuendelee kuwaelimisha kuwa Wananenepesha tu Matumbo ya Mafisadi!!:A S angry:
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…