Kweli hapana pana penzi au nighairishe

Isalia

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2011
Posts
1,209
Reaction score
435
Nimekaa na mchumba wangu tukipiga stori za hapa na pale katika mazungumzo alikusudia kutaja jina langu lakini akataja jina la mwanaume mwengine mwenyewe akajishitukia na kuniomba radhi kwa mtazamo wangu hana mapenzi na mimi iweje anite jina la mwengine kiukweli na wacwac nae na kutaka kughaira haruc yetu je itakua nimemtendea haki
 
uatakiwa kwanza kujua huyo alietajwa ni nani...
je kama ni marehemu?
unatishwa hata na marehemu?
 
Mmh mapenzi bana...bora nilieamua kukaa pembeni.
 
kama kamtaja wakati mnapiga story tu it is not a big deal; ngoma ingenoga kama angemtaja mkiwa katikati ya game
 
kutaja jina la mwanaume kwenye maongezi siyo shida, inategemea huyo mwanaume anafahamiana vipi na mchumbako. Huenda wamezoeana ktk mazingira ya kazi nk. ingekuwa ametaja wakati wa kunanihii.. yangekuwa mengine.
 
Yaani wewe ni wa kuzugia tu mwenye chake ni yule aliyetajwa!
Tafakari..... chukua hatua.............ngeeeeeeeeee
 
kwa maongeze tu cdhani kana ni isue sana......kama vp inabidi umjue huyo ni nani.
 
Nighairishe? Hapana! NIGHAIRI ndiyo sahihi.
 
Yaani wewe ni wa kuzugia tu mwenye chake ni yule aliyetajwa!
Tafakari..... chukua hatua.............ngeeeeeeeeee

duh, mkuu utamuua mwenzio kwa presha aisee ingawa kuna kaukweli kidogo ndani yake
 
Ongea nae kwanza ujue mtu huyo ni nani na wana uhusiano gani,kabla hujakimbilia kumhukumu na kufanya maamuzi ambayo huna uhakika na kosa lenyewe!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…