Pangaea
JF-Expert Member
- Jun 14, 2012
- 202
- 41
WanaJF.
Nipo kando ya TV ninafuatilia majadiliano bungeni. Ninaona waheshimiwa kadhaa wananadai nchi hii itaendelea iwapo Kiswahili kitaenziwa. Ninatambua umuhimu wa lugha kama chombo cha mawasiliano na nionavyo hapa Tanzania hatuna tatizo la uelewa wa Kiswahili. Pia sheria, vitabu vya kufundishia nk vinaweza kuandikwa kwa Kiswahili ili wasiofahamu Kiingereza waweze kufahamu. Lakini siamini kama kuuondoa Kiingereza na kubaki na Kiswahili peke yake si sababu ya kuondoa umaskini, kuboresha elimu, kuleta haki na usawa katika nchi, kukuza uzalendo. Jambo la msingi ni kuboresha elimu ya Tanzania- maslahi ya waalimu, mazingira ya shule, vyuo vinavyofundisha walimu (hasa vyuo vikuu) na sifa za kuwa mwalimu zitizamwe (mtu ambaye hajapata mafunzo ya ualimu asirusiwe kufundisha kama ilivyo sasa), mitaala iboreshwe nk. Siamini kama nchi za wenzetu hazifundishi lugha za kigeni. Suala ni ubora wa elimu. Ninaomba kuwasilisha.