Kweli Kiwango cha soka kimeshuka Mno

ibanezafrica

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
7,261
Reaction score
6,553
Nimesikia leo wachambuzi E fm wakimhoji mchezaji wa zamani,point moja ilionigusa ni pale iliposemwa kua mchezaji 'Malota soma'ball jagural"pamoja na weledi wote alokua nao hakuwahi cheza National team na hii yote ilitokana na viwango vya wachezaji wengi wakati huo kua juu sana!kitu ambacho leo mchezaji anaweza ibuka from nowhere ukamsikia yumo taifa stars!ukiangalia rank za fifa za miaka ya 1984 kurudi nyuma hadi 70s tulikua pazuri mno,nina imani timu ya Umiseta combine ya Mashariki na ile ya Magharibi za mwaka 1986-88 ni bora zaidi ya timu za sasa za Yanga,Simba na Azam ki uwezo japo timu zile za shule hazikutumia walimu/coach wa kigeni'wazungu'hebu tutafakari hili na wengine tuzungumzie soka lile tamu...
 
Ulichosema ni sahihi lakin kutochaguliwa malota soma timu ya taifa haikumaanisha kuwa waliocheza au walioitwa katika namba yake walimzidi uwezo no ni mfumo na mapenzi ya makocha ,innocent haule,peter tino ndio walikua wanachuana katika namba ya malota pamoja na edward chumila....
 
Nimefurahi walau umebadili mada dah maana ni siasa tupu nw mpaka inachosha sasa.. Swala lako naona hapo baadhi ya makocha huchugua wachezaji jinsi watakavyo wao ila c ubora wa mchezaji hili ndo linaifanya timu yetu ya taifa kuwa hvi mpka sasa kwa sabab ya upuuzi wa baadhi ya makocha wamekuwa wakiiwaacha wachezaji wazur na kuchukua wachezaji wabovu kisa tu wajulikana bila kuangalia kiwango chao kwa muda huu...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…