Magulumangu
JF-Expert Member
- Jan 7, 2010
- 3,051
- 461
Nilitamani sikia,kwaheri tokea kwako,
Japo ulikuwa malkia,shambani hekima kwako,
umasikini nasikia,ulitoa uhai kwako,
Kweli mama umeenda,naenzi mapenzi yako,
Amani ulihubiri,fisadi wamepokonya,
ungesema mahafari,sio hasi ningefanya,
lako juu kaburi,mshumaa ulo nyanya,
Kweli mama umeenda,naenzi mapenzi yako,
sipitali kuchelewa,kunipenda uliwahi,
mdomoni yalinenwa,kabla ya ile subuhi,
ni kipindupindu hewa,walisema asubuhi,
kweli mama umeenda,naenzi mapenzi yako,
Angekuwa mama salma, tume huru ingeundwa,
wangeenda alabama,uhai wake okolewa,
mindege dalisalama,radio ingetolewa,
Kweli mama umeenda,naenzi mapenzi yako,
Cha kujivunia sina,zaidi ya yale mapenzi,
maneno yako si hina, kufutika kama tenzi,
sasa nimeyaona,ulonichangulia wangu mwenzi,
kweli mama umeenda,naenzi mapenzi yako,
Wivu daima ulija,kama alo mungu kwetu,
ulimuonya hata shija,husu sisi chama chetu,
akakuona wa kuja,kwa kujiona yeye chatu,
Kweli mama umeenda,naenzi mapenzi yako,
Mwangaza ulikuwa,giza lilipotanda,
mkate si uliliwa,kila kitu kimepanda,
wako huko ihumwa,bajeti iko kitunda,
Kweli mama umeenda,naenzi mapenzi yako,
Baba pia ateseka, kwa nini ulimwacha,
ile ahadi mulitaka,timie kila kukicha,
kukufata anataka,anaogopa wale mapacha.
kweli mama umeenda,naenzi mapenzi yako,
Japo ulikuwa malkia,shambani hekima kwako,
umasikini nasikia,ulitoa uhai kwako,
Kweli mama umeenda,naenzi mapenzi yako,
Amani ulihubiri,fisadi wamepokonya,
ungesema mahafari,sio hasi ningefanya,
lako juu kaburi,mshumaa ulo nyanya,
Kweli mama umeenda,naenzi mapenzi yako,
sipitali kuchelewa,kunipenda uliwahi,
mdomoni yalinenwa,kabla ya ile subuhi,
ni kipindupindu hewa,walisema asubuhi,
kweli mama umeenda,naenzi mapenzi yako,
Angekuwa mama salma, tume huru ingeundwa,
wangeenda alabama,uhai wake okolewa,
mindege dalisalama,radio ingetolewa,
Kweli mama umeenda,naenzi mapenzi yako,
Cha kujivunia sina,zaidi ya yale mapenzi,
maneno yako si hina, kufutika kama tenzi,
sasa nimeyaona,ulonichangulia wangu mwenzi,
kweli mama umeenda,naenzi mapenzi yako,
Wivu daima ulija,kama alo mungu kwetu,
ulimuonya hata shija,husu sisi chama chetu,
akakuona wa kuja,kwa kujiona yeye chatu,
Kweli mama umeenda,naenzi mapenzi yako,
Mwangaza ulikuwa,giza lilipotanda,
mkate si uliliwa,kila kitu kimepanda,
wako huko ihumwa,bajeti iko kitunda,
Kweli mama umeenda,naenzi mapenzi yako,
Baba pia ateseka, kwa nini ulimwacha,
ile ahadi mulitaka,timie kila kukicha,
kukufata anataka,anaogopa wale mapacha.
kweli mama umeenda,naenzi mapenzi yako,