white wizard
JF-Expert Member
- May 18, 2011
- 8,566
- 13,770
Jana katika maeneo ya mivinjeni,mwendesha pikipiki mmoja ameibiwa pikipiki na demu!!picha yenyewe ilikuwa hivi. Huyo demu alishakuwa na mazoea na huyo dreva wa bodaboda yapata wiki 2 hivi.
Na huyo demu akija hapo kuna bar anampa jamaa offer kisha anamkodi anampeleka, kumbe huyo demu anajenga mazoea kwa jamaa, na ulikuwa ukiwakuta utadhani ni mtu na mpenzi wake, sasa jana demu akamwambia leo naendesha pikipiki mimi, jamaa c amesha kolea na ndio walikuwa wamepanga ndio cku ya kula tunda!
Jamaa akakaa nyuma demu akaanza kuendesha kwenda guest house moja, kufika mbele demu akajifanya kudondosha kiatu alichokuwa amevaa, na kulikuwa na umbali na pale aliposimamisha pikipiki,
na ilikuwa mida ya saa mbili usiku, jamaa akashuka kuchukua kile kiatu cha bibie,. Akawa amefanya kosa la jinai yule demu aliiondoa pikipiki hiyo kwa kasi ya ajabu,.
Jamaa akabaki analia tu nitamwambiaje bosi wangu pikipiki yenyewe hata mwezi bado. Jamaa akaenda kutoa taarifa kituo cha polisi Kilwa road. Na yule demu inaonekana ni mtaalaam sana kwenye mambo hayo kwani hiyo speed aliyotoka nayo hapo!
JAMANI TUWENI MAKINI CKU HIZA WANAWAKE NDIO WANATUMIKA KWENYE WIZI, KWANI NDIO UDHAIFU WA WANAUME.