kweli mapenzi na kazi noma!!!!jamaa aibiwa pikipiki na demu!

white wizard

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2011
Posts
8,566
Reaction score
13,770
Jana katika maeneo ya mivinjeni,mwendesha pikipiki mmoja ameibiwa pikipiki na demu!!picha yenyewe ilikuwa hivi. Huyo demu alishakuwa na mazoea na huyo dreva wa bodaboda yapata wiki 2 hivi.

Na huyo demu akija hapo kuna bar anampa jamaa offer kisha anamkodi anampeleka, kumbe huyo demu anajenga mazoea kwa jamaa, na ulikuwa ukiwakuta utadhani ni mtu na mpenzi wake, sasa jana demu akamwambia leo naendesha pikipiki mimi, jamaa c amesha kolea na ndio walikuwa wamepanga ndio cku ya kula tunda!

Jamaa akakaa nyuma demu akaanza kuendesha kwenda guest house moja, kufika mbele demu akajifanya kudondosha kiatu alichokuwa amevaa, na kulikuwa na umbali na pale aliposimamisha pikipiki,

na ilikuwa mida ya saa mbili usiku, jamaa akashuka kuchukua kile kiatu cha bibie,. Akawa amefanya kosa la jinai yule demu aliiondoa pikipiki hiyo kwa kasi ya ajabu,.

Jamaa akabaki analia tu nitamwambiaje bosi wangu pikipiki yenyewe hata mwezi bado. Jamaa akaenda kutoa taarifa kituo cha polisi Kilwa road. Na yule demu inaonekana ni mtaalaam sana kwenye mambo hayo kwani hiyo speed aliyotoka nayo hapo!

JAMANI TUWENI MAKINI CKU HIZA WANAWAKE NDIO WANATUMIKA KWENYE WIZI, KWANI NDIO UDHAIFU WA WANAUME.
 
Mmh!Ama mapenzi makirikiri, nadhani huyo jamaa aliyasahau ya ngoswe mzee wa masarawili.."PENZI KITOVU CHA UZEMBE"
 
Kudadadeki.., sasa jamaa kumkimbiza alishindwaje??
 
Huyu demu ni mafia aisee!
 
Mkuu weka habari yako vizuri. pale mvinjeni guest ziliyopo ni siku na olympic. na bar iliyopo ni pentagon na ile ya pale nyuma yake kweye kitimoto relini. ile barabara inayoenda zilipo guest house haitoki, sasa aliwezaje kukimbia na pikipiki maeneo yale?

Nieleweshe mkuu.
 

Walikuwa wanatoka bar ya pentagon mi nilikuwa maeneo ya ufundi kwenye petrol station ya bp,ndio pale nikaona pikipiki inasimama,na jamaa anatelemka anakimbia kuelekea chini.

Ndipo yule demu akaondoa pikipiki,akavuka barabara kuelekea kwenye kota za polisi kuna njia inakatisha pale,kulingana na maelezo yake alisema walikuwa wanakwenda kwa azizi ali, ila rafiki yake naye ni dreva wa bodaboda alipofika ndio akatoboa siri yote,na walikuwa wanakwenda guest house(IKWETA)kwa azizi ally!
 
hapo sawa. ngoja ntawauliza madreva pick up hapo ufundi ili nipate uhakika. hii habari nmeipenda sana. hadi mamafia wamefika bongo!. hii ni hatari sana. kama kaelekea keko pikipiki hataipata.
 
Kaazi Kweeli kweeli ......!!!!!!!!!

Madem wengine ni majambasi sana.

Kama huyo anakukuta peke yako mitaani usiku unafikiri waweza pona? Jihadhari na madem usio wajuwa.
 
Ngoja na mimi nizidishe umakini wasije wakalamba Bajja langu mbona ntalia mimi !!
 
Mambo ya changu Mimi wewe pia chako hayo,mwambie asilie mjini shule.
 
jamaa alikuwa kajiaanda kwa game! Teh teh teh, kesho yaweza kukupata ww, usimwamin m2, hasa nyie wenzangu mnaowafungia watu ndan
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…