Kweli mapenzi ni mental disease

Kweli mapenzi ni mental disease

Sisa Og

JF-Expert Member
Joined
Apr 18, 2024
Posts
201
Reaction score
504
Kipindi nasoma shule, nilipata kumsoma jamaa anaitwa Plato. Sikumbuki mengi sana kumhusu, ila nakumbuka kauli yake "Love is serious mental disease" na hii nimeishuhudia mara mbili kama ifuatavyo:
* Hapo nyuma, nilitumwa na wazazi wangu niende kumlinda (spying/stalking) sister yangu ambae alikuwa anapitia kipindi kigumu sana.
Alikuwa ameachwa na mchumba wake ambaye alikwishamleta mpaka home. Maisha yalikuwa magumu sana. She had everything: house, car, good job but all sounded nothing.
Nilikuwa napika hali, anakaa chumbani amejifungia, aliacha hadi kuoga na kubadili nguo. Nilipoona nazidiwa nikapiga simu nyumbani akaja mtu mwingine (sister) kumcheki.
Baada ya hapo nilienda kujiunga na shule. Nilikaa huko mwaka bila kumuona nilipomuona alikuwa ameshakuwa sawa. Lakini hataki kusikia neno mapenzi.


* Niliporudi shule ndo safari yangu ikaanza. Nilishadate na wadada kadhaa hapo nyuma lakini nilikuja kugundua wote hao nilikuwa nacheza. Hii ni baada ya kukutana na huyu shemeji yenu aliyenifanya niandike uzi huu.
Nilimpenda sana tu mara ya kwanza kumuona. Kwakuwa alikuwa ni mgeni niliforce urafiki naye kwanza. Sikuchelewa nikatema swaga. Sikuamini kama ningetoboa. Lakini nilifanikiwa.
Muda ulivyozidi kwenda nilizidi kumpenda sana.
Tulipotezana miaka mitatu, nikaja kukutana nae tena. Lakini hiyo miaka yote nilishindwa kupata mahusiano ya kudumu. Kila mrembo niliyedate nilikuwa namchukia na kudhani namsaliti mpenzi wangu ambaye sijui yuko wapi.

Mpaka sasa napitia kipindi kigumu kwenye maisha yangu. Nimekuja kugundua huyu mrembo wangu hanizingatii tena kama zamani. Nilidhani kwa kuwa tumepotezana miaka yote hiyo basi atakuwa amenimiss sana. Lakini mwenzenu sipendwi tena. Nimejaribu kila njia arudi kwenye line lakini nimekata tamaa.
Nashindwa kula, stress kibao tu. Imefika hatua nachukia kila mtu, napenda mziki ila sioni hata nyimbo za kusikiliza. Juzi nilianguka sababu ya kizunguzungu.
Lengo langu nataka nimsahau, tafadhari aliyewahi kupitia feelings kama hizi aliwezaje? Ni njia gani sahihi kumsahau mtu. Hata nikisema nifute picha na namba yake kazi bure kichwani taswira yake naiona. Mbaya sana hapa ninapokaa kuna jirani yangu anaitwa jina kama lake yani natamani kuhama.
Asanteni.
 
Na bado
Utanyooka tu...
Mapenzi tunaendekeza tu
Furaha ya maskini NGONO
UWEZI KUTA ELON MUSK,JEFF Wanateseka kuwaza mapenzi
 
Pole sana
Anza pia kuongea na Dada aliyeyapitia atakueleza iweje uso kwa uso.
 
Na bado
Utanyooka tu...
Mapenzi tunaendekeza tu
Furaha ya maskini NGONO
UWEZI KUTA ELON MUSK,JEFF Wanateseka kuwaza mapenzi
Kiongozi, we acha tu. Mimi sio tamaa ya ngono. Bora ingekuwa tamaa ya ngono maana nchi hii kupata ngono ni rahisi kuliko kupata hela
 
Mwanangu demu akikukataa mtafute mkali zaidi yake apo utapona mapema sana# nay wa mitego

Kingine hii inawakutaga masela wenye demu mmoja move on br. Kwann ujiumize kwenye hamna wakati maisha yenyew mafupi
 
Back
Top Bottom