Kweli Marehemu Christopher Mtikila alisema kweli kuhusu 'unyani'

Kweli Marehemu Christopher Mtikila alisema kweli kuhusu 'unyani'

daza steven

JF-Expert Member
Joined
Aug 30, 2016
Posts
359
Reaction score
358
Marehemu christopher Mtikila alikuwa akilia sana na kuwafananisha viongozi wa Tanganyika wakati ule na viongozi wa Afrika na nyani ambao tunawaona mstuni. Marehemu Mungu ampe pepo ya milele. Mchungaji alienda mbali sana na kusema viongozi wa Afrika wako tayari kuuza ndugu zake, familya yake, ukoo wake, watu wa nyumbani kwake, jamii yake eti kwa Harua na tende.

Mchungaji huyo ambaye alikuwa gwiji la siasa za upinzani ambaye alikuwa amung'unyi maneno na alikuwa anatembea katika mstari aliwai kusema hawa viongozi manyani ambao kwa maumbo wapo kama binadamu wanaweza kuuza chochote au kukubali shariti lolote kutoka kwa mabeberu kama akipewa kitu kidogo.

Hotuba yake hiyo ambayo ilikuwa ukiisilikiza kwa makini lazima utoe mchozi leo tunawaona hawa maraisi manyani Afrika wazi wazi wakikubali kuongeza janga juu ya janga juu ya janga, ni manyan tu.

Leo hii tunashuhudia maraisi wengi wa Kiafrika wakicheza nyimbo za wazungu kwa kupambana na Covid 19 kama wanavyopambana mataifa ya dunia ya kwanza kisa wamehaidiwa mpunga kutoka WHO Shirika la Afya Duniani.

Tumeshuudia wananchi katika mataifa mbali mbali wakilalamika chakula cha msaada kuto wafikia na hata kikiwafikia chakula ni kidogo sana hakiwatoshi na ni chakula cha aina moja yaani kama maindi maindi tu. Unaweza kushangaa kivipi mtu ale maindi makavu hayajasagwa, hakuna mboga, tumeshuudia wananchi katika nchi mbalimbali wakilalamika sana.
Sijui sisi Waafrika ni nani aliye tuloga kwani mtu yupo tayari wananchi wake waadhirike kabisa kisa yeye kapata mzigo kidogo kutoka kwa wazungu hili si jambo zuri na si utamaduni mzuri kwa Waafrika ifike wakati sasa tuseme basi.

Pia tumekuwa na baadhi ya madaktari au wataalamu wa afya manyani vilevile hapa Tanganyika kwa jinsi walivyokuwa wanalishughulikia swala la ugonjwa huu, yaani wamekuwa wanalalia sana elimu ya kizungu bila kujua wapi walikotoka wakisema barakoa lazima zitoke Ulaya, na kufikia baadhi ya madaktari wetu mabofaloo docta kutokukubaliana na dawa za asili kama kujifukiza wakati hao wazungu mpaka hapa naandika bado hawajagundua dawa.

Hawa wataalamu baadhi ambao ni manyani pia, wamekuwa wakihusisha kila kifo na Korona hata kama mtu kafa na TB au Presha, walianza kuzika watu usiku na kupora misiba kanakwamba wamekuwa wazee wa mila wa Umofia.

Utaweza kushangaa kuona mataifa ya Ulaya, Amerika na Asia wameanza kulegeza mashariti na kukiri kuwa njia ya kupambana Korona kwa kufungia watu ndani haiwezekani, lakini viongozi wengi wa Afrika bado wanalivalia bango swala la kufungia watu ndani na hata hapa Tanganyika tunao hao viongozi manyani wanataka Watanzania wafungiwe ndani hadi wakome tena kutoka upinzani hatujui kama wangechukua nchi wangetuumiza zaidi, ni Mungu katunusuru.

Wewe ukiwa unaunga mkono watu wafungiwe hili wafe na nja wewe ni nyani tu nyani kasoro mkia.

Nachukua fursa hii kumshukuru Mungu hapa Tanzania kwa kutupa Raisi binadamu na si nyani huyu Mzee wa Chato hakika ni binadamu yeye amenyimwa pesa na WHO kisa hajafungia watu wake ndani.

Namalizia kwa kumbariki Mchungaji Kristofa Mtikila kwa maombi yake ya kulaani unyani hata sasa Tanganyika tuna Rais binanadamu kabisa, si nyani kama baadhi ya maraisi na kiongozi wetu mmoja wa upinzani ambaye hadi sasa ameshikiria bango kulokudouni ni nyani tu.

Si maneno yangu bali ni ya Mchungaji Kristofa Mtikila alale mahara pema kwa baba.
 
Viongozi wengi wa Africa ni brainwashed

Wakimuona muzungu meno yote nje Angalia mfano Kenyatta Au Chadema yaani kwao muzungu ni km Mungu
 
kuzunguka kote huko mara leo umombee pepo Mtikila ambaye kifo chake huenda kimetokana na magumashi ya chama chako.ni ili tuu ulambe nyayo za mfalume wenu sie tunajua mmekataa lock down kwakuwa nchi iko dhoofulhali mnajua mkiwafungia nusu nzima ya raia wenu itakufa njaa haswa wana CCM ambao wengi hawako na uwezo wa kifikra na ni masikini sana wa kipato na akili
 
kuzunguka kote huko mara leo umombee pepo Mtikila ambaye kifo chake huenda kimetokana na magumashi ya chama chako.ni ili tuu ulambe nyayo za mfalume wenu sie tunajua mmekataa lock down kwakuwa nchi iko dhoofulhali mnajua mkiwafungia nusu nzima ya raia wenu itakufa njaa haswa wana CCM ambao wengi hawako na uwezo wa kifikra na ni masikini sana wa kipato na akili
Du sijakuelewa ndugu, haupo Tz nini, tunalokiwa kichama au sijakusoma
 
Back
Top Bottom