Kweli mke wa mtu ni sumu

Manyanza

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2010
Posts
16,464
Reaction score
35,629
Wakuu !
Habari za majukumu na mishemishe za maisha ya kila siku ?

Huu msemo wa Mke wa mtu ni sumu hakika ni kweli na ni sumu kweli pale utakapo ingia kwenye 18 za mwenye mke wake.

Kuna visa kama vitatu hivi nitavielezea hapa, viwili nimevishuhudia kwa macho yangu na kimoja nilisimuliwa na Mshikaji wangu ambaye ni fundi umeme.

Kisa cha kwanza nilicho kishuhudia kwa macho kilitokea maeneo ya Buguruni kama miaka 8 iliyopita. Ilikuwa hivi kuna Kijana alikuwa ni Mwalimu alikuwa akiwafundisha watoto wa Jamaa Tuition, kila siku jioni alikuwa anaenda kuwafundisha wale watoto, sasa baada ya muda kidogo jamaa akajenga mazoea na mke wa Jamaa na Jamaa mwenye mke alikuwa ni mfanyabiashara mwenye ishu zake Kariakoo. Katika mazoea ya hapa na pale Teacher akaanza kumla mke wa jamaa tena mle mle ndani na alikuwa na mazoea ya kwenda kujilia tunda muda wowote hata pale Watoto wanapokuwa wapo shule yeye amachukua bodaboda anaenda kushusha mzigo.

Siku zilienda mpaka majirani wakawa wameshitukia ule mchezo ikabidi wamtonye mwenye mke. Mwenye mke kwa sababu alikuwa anampenda sana Mke wake ikabidi ampige marufuku Mwalimu kuja kuwafundisha watoto tuition pale nyumbani.

Mawasiliano kati ya Mwanamke na Teacher yaliendelea huku jamaa mwenye mke alikuwa amewapa kazi Vijana ya kufuatilia nyendo za mke wake.

Za mwizi ni 40 tu, siku ya tukio na Mimi siku hiyo nilikuwa maeneo ya Buguruni kwa sababu nilikuwa na mshikaji wangu maeneo yale. Ilikuwa ni jumamosi mida ya saa 7 mchana wakati fumanizi linatokea tupo Bar na Mshikaji wangu mara kelele na vurugu za hapa na pale zikatokea.

Hiyo Bar ilikuwa na Guest House mle mle, ghafla upande wa guest house tukasikia kelele na vurugu, jamaa mwenye mke alikuwa ameweka mtego na akawa amewakamata mgoni wake na mke wake, Jamaa alikuwa analia sana kwa sababu baada ya kumfumania mke wake wake alipovamia alilizwa na ule mkuyenge wa ticha 🤣🤣🤣

Ticha alikuwa na mguu wa mtoto na jamaa aliuona live aliishia kulia kwa hasira sana. Kama mnavyojua fumanizi la Uswazi watu huwa wanajaa kama kuna harusi ghafla difenda la polisi likaja pale likawabeba Mwanamke na yule jamaa mpaka kituoni, baada ya hapo sikufuatilia tena.

Tukio la pili hili nilisimuliwa na jamaa yangu Fundi umeme hili lilitokea maeneo ya Mbezi Msumi. Kuna Kijana alikuwa anamla mke wa mtu yaani mwenye mali akitoka tu na mwizi wa mali anaenda kujipakulia mke wa mtu. Kuna siku jamaa kama bahati tu aliongea na mlinzi wake Mmasai akampa na hela na Mmasai akaropoka kuna njemba huwa inakuja hapa mapema tu saa moja au saa mbili asubuhi ukiondoka kwenda kwenye mishe zako, Jamaa akamwambia Masai chukua hii 5000 weka vocha akitokea tu huyo mwizi wangu nipigie.

Kumbe jamaa baada ya kuambiwa vile akawa amewapanga wale Majamaa ya Naccoz Camp Gym pale Mabibo kwa Mfaume Mfaume yule Bondia. Siku ya tukio la kukamatwa mwizi ilikuwa mida ya saa 6 mchana, Masai alimpigia Bosi wake na Bosi akawasiliana na wale jamaa wa Naccoz Camp wakavamia walimkuta Mgoni yupo na taulo tu sebuleni anasubiri kunywa mchemsho wa Kuku.

Jamaa alipovamia na wale Mabaunsa hawakuwa na stoy nyingi sana wale Mabaunsa walitengewa ule msosi na wakanywa na bia safari lager za kutosha.

Baada ya kushiba walimkamata yule mgoni walimshughulikia haswaa mpaka aliacha kinyesi na wakaambiwa Mke na Jamaa wapige deki. ( Hii ni story niliambiwa na jamaa yangu )

Tukio la tatu nililoshuhudia ni juzi mechi ya Simba na Yanga.

Kuna Mshikaji ambaye ki umri ni age-mate wangu tu (34, 35, 36) alikuwa na mazoea sana na Dada mmoja hivi ambaye ni mke wa mtu huyo Dada ni muuza duka la mumewe. Mshikaji alijenga naye mazoea yaliyopitiliza mpaka wakati mwingine alikuwa anamkumbatia hadharani.

Aisee vile vitendo tulikuwa tunamwambia sana achana na haya mambo hata kama unakula huo mzigo usijionyeshe hivyo. Siku ya Jumamosi (Simba na Yanga Day) ndio walikuwa wamepanga wakapeane utamu. Kwa sababu yule Dada ni Msabato alikuwa hafungui duka.

Walipanga wakutane lodge na jamaa alikuwa na kimuhe muhe sana.

Demu alitangulia lodge na jamaa akamfuata yule Demu. Kufika lodge akampigia yule demu na demu akamwambia nipo room no fulani. Jamaa naye akaenda mpaka ile room akafungua mlango na kuingia ndani, ile anafunga mlango tu nyuma ya mlango alikuwa amesimama Mwenye mke na Chooni kulikuwa na Jamaa mwingine. Na Mwanamke alikuwa amekaa kitandani.

Lakini mpaka sasa huyu Mshikaji haonekani hapa mtaani na sijui ilikuwaje huko lodge, na Mwanamke yupo dukani anaendelea na kazi zake poa kabisa na yuko happy as usual.

Hitimisho:
Wake za watu hawafai Vijana wenzangu tuachane nao na tusiwe tunatengeneza mazoea nao hata kidogo. Unaona Mwanaume mwenzako anatunza na kuhudumia na wewe unataka mserereko acha kabisa mazoea na Mke au Mpenzi wa mtu ni hatari, fedheha na aibu.
 
Mke wa mtu nae ni mtu mzima mwenye meno 32 nae ana maamuzi yake.

Binafsi naona mkichapiwa wake zenu, mfikirie kuna kitu mtakua mnalega ndio maana umechapiwa na sio kuvimba na mchapaji ,sio suluhisho la kuepuka kuchapiwa🤔
 
Mke wa mtu nae ni mtu mzima mwenye meno 32 nae ana maamuzi yake.

Binafsi naona mkichapiwa wake zenu, mfikirie kuna kitu mtakua mnalega ndio maana umechapiwa na sio kuvimba na mchapaji ,sio suluhisho la kuepuka kuchapiwa🤔
Acha kuwashawishi na kuwapa hamasa za kijinga vijana nao watakuwa na wake pia
 
Naomba tu niseme kwamba binafsi napotongoza mwanamke swali la kwanza huwa nauliza kama ameolewa alinambia hvo hiyo ndo bye bye Ila hakisema no lazima achezee mkuyati mambo mengne mbele kwa mbele

NB. Si mfuasi wa Kula wake za Watu na wewe unaekula wake za Watu Usijali "parachute" linakuhusu muosha huoshwa

Mwisho hivi mdudu anaingiaje kwenye tunda ambalo halina Ata tobo
Jibu ni kwamba "it was process since lile tunda lilipokuwa kama ua" kwahiyo wa kulaumiwa hapa ni mwanamke
 
Mke wa mtu sumu linajulikana lakini tatizo linakuja wanandoa wengi saana wanaishi kama kaka na dada yaani wakishaoana tu hata zile pigo alizokuwa anapewa wakati wa uchumba hazipati tena sasa akikutana na mwamba huko nje ndipo kimbembe kinaanza hakubali kumuacha mwamba yuko radhi hata kuhonga aendelee kupata huduma anayokosa kwa mmewe
 
Dah! kinachotuumiza wanaume ni unawaza jinsi unavyomkunja mkeo,mambo ya fore play, Bj n.k unawema inamaana ile njemba inamfaidi kama ninavyomfaidi my dia waifu? Hapo utachanganyikiwa ndo maana wengine wanaua kabisa, alafu ukute bahati mbaya una maumbile madogo utawaza pengine mke simridhishi
 
1. Namba moja sijaona sumu hapo, je mwenye mke kulia au kupelekwa polisi ndio sumu?
3. Huu ni uongo, uongooo, jamaa haonekani wewe haya yote umesimuliw na nani?
 
Usione aibu kama kuna lolote limetokea kijana

Tutakufariji na kukutia moyo,eleza tu.🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…