Kweli nimeamini CCM ni chama cha wakulima na wafanyakazi

BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2019
Posts
377
Reaction score
435
CCM inajidhirisha kwamba ni Chama cha Wakulima na Wafanyakazi na hiyo ni baada ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo kuagiza Serikali kununua mahindi yote zaidi tani 100,000 katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini baada ya bilioni 14 zilizotolewa awali kununua tani 24,000 za mahindi kuisha.

Kama hiyo haitoshi, CCM imeiagiza Serikali kukaa na haraka kupunguza bei ya mbolea huku ikisisitiza bei ya mahindi iwe ile ile kila mahali kwa walio mbali na karibu.

Mwisho Katibu Mkuu Chongolo anamaliza kwa kusema ndani ya wiki mbili, CCM itaanza kufuatilia utekelezaji wa maagizo hayo.

Ama kweli nimeamini CCM ni Chama cha Wakulima na Wafanyakazi. Hakuna kero ya Mkulima na Mfanyakazi wa nchi hii itakayoachwa.

Bwanku M Bwanku

0657475347

Your browser is not able to display this video.
 
CCM wewe unayoijua leo imebadilika sana toka uasisi wake.

Enzi za Mwalimu ndo chama kilikuwa cha wakulima na wafanyakazi.

Tulifikia hadi kuwa na mwenyekiti wa chama dikteta ambaye anafanya anachoamua na kujua mwenyewe.
CCM has never been the same.

Tafuta wakulima au wafanyakazi ndani ya CCM na utashangaa kama ule uwakilishi uliotazamiwa wakati wa uasisi kama upo.

Sasa hivi CCM inaendeshwa na watendaji toka serikalini kama kina Chongholo.
CCM ni idara ya Serikali Kuu
 
Duh! Hii nafasi Ya Katibu Mkuu Inapitia kipindi cha Mpito ambapo ni Kama imejificha kwenye Vyama karibia vyote Hawasikiki Kabisa. Yaani Yule Wa CCM kumbe anaitwa CHONGOLO! sijui wa CDM anaitwa nani?

Makatibu Viiipi ? Tulishazoea hizo ni nafasi za amsha amsha!
 
Umerogwa wewe. Chadema ni lini walipandisha Bei ya pembejeo?
 
Serikali imeua siasa. Inataka itawale kidikteta
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…