Kweli yenye mwanzo yana mwisho nikukumbuka ubabe wa hawa wasanii

Umemsahau Chid benz aliwahi kumkunja tai na kumtisatikisa Pr Jay mh. Mbuge now. Kwa sasa Chid benz anahangaika na dunia
 
✅Muda ni Noma Kiongozi nakubaliana na mdau hapo juu kwamba si kwa wasanii tu ni katika nyanja zote,enzi hizo elimu ilikuwa elimu kulikuwa na wakali hadi inatisha,kuna watu walitisha kwenye Elimu mmoja wapo ni Ngaimisi wa Mzumbe alifunika mbaya na alibuluza hatari lakini matokeo yalivyotoka Ngaimisi hayupo hata top 10 na kapotea mpaka leo,Nakumbuka kulikuwa na ma TO walijulikana Tanzania nzima leo hii ni hatari tunadandia nao madaladala,wapi Wenzi Man?

✅Kulikuwa na Msanii Mr Nice,ni mtoto yupi kipindi Chake alikuwa hajui kuku kapanda baiskeli? Kikulacho? Rafiki? Mama? Mr Nice alikuwa anatembea na Msafala wa Magari na Mabaunsa utafikiri ni raisi,Mr Nice alikuwa anajaza uwanja commoro,Uganda,Mr Nice alikuwa ana sold out shows account yake ilifikia hadi bilioni 1.5 enzi hizo kwa rate ya sasa unaweza ukasema value yake kama bil 6,Mr Nice alikuwa kila asubuhi anakuja kuamshwa na warembo kisha wanamfanyia message,Nyumbani kwake sinza ilikuwa tafrani kwa majirani kila siku ilikuwa block party mziki mnene,Leo Mr Nice anaishi kama DigiDigi haonekani kabisa.

✅Enzi Zetu tunakua kulikuwa na Wababe hasa kina Van Damme, Sancho La Tino Leo,Ukikutana na Damme njiani ilikuwa unasali maana ilikuwa mawili akuzimishe au uondoke huna hata senti tano,Leo hii Van Damme teja si teja,mlevi si mlevi ,kareti zote zimekwisha hata panya road m1 wa miaka 15 anamfloatisha wakiweka paling.

✅Ni kweli matter of time hata huyu unayeona anang'ara Leo mda utaongea tu,si Diamond ,Si fela,Si Ruge Si Majizo wote watapokeza vijiti kwa wenzao,Waulize wazee wa zamani watakueleza kuhusu kina Mbaraka Mwishee walivyotikisa,Waulize kuhusu Mohamed Kipande,Waulize kuhusu Eddy Shaggy Milima ya kwetu walivyotisha,Leo imebaki story.

✅Je unakumbuka kina Jordan enzi zao kwenye ballin? Unakumbuka Tyson akifanya pambano Las Vegas Nevada tulikuwa tunaamka saa tisa kwenda kucheck pambano ilikuwa hakuna kulala, unakumbuka Michael Jackson kipindi thriller inatoka 1986? ilikuwa balaa yani ni hatari,hapo ndipo napokumbuka mistari wa Camron Dipset akimdiss Nas kwamba "HIS CAREER IS OVER LIKE MIKE ANYONE JORDAN,TYSON,JAKSON." Ni matter of time.

✅Ukija Kwenye Siasa kulikuwa na wanasiasa wenye mvuto Hatari,kuna mwanasiasa mmoja ni mbunge nakumbuka ilikuwa akisimama kwenye jukwaa watu walikuwa wanalipuka kwa shangwe la kufa mtu,alikuwa na mvuto hata kwenye social media akitoa status yeyote watu wanamsupport na macomments na malikes ya Hatari,Leo hii akifanya mkutano akizidisha hata watu 100 sijui labda afanye jimboni kwake,Leo hii akiandika wazo kwenye mtandao wa kijamii inaweza ikapita hata masaa 6 hana hata comment hata moja ni hatari sana.

✅Zembwela anakwambia Mda au Nyakati ni HATARI ,Je unakumbuka Ze Commedy ilivyobamba enzi zake EATV ,Nani alikuwa anakosa kila alhamis jioni kuangalia mdebwedo wa kubonyeza kizenji bonyeee? Nani alikuwa anakosa kuangalia Tajiri la Kihaya? Mda unaongea wote wamepotea wengine ni wachungaji,wengine watangazaji,wengine wamejikita kwenye matangazo ya TV/Radio.Swala hapa ni career iliyokupa umaarufu na kujulikana na ikabamba hata kama sasa unafanya issue nyingine lakini Haipo kwenye spotlights.

✅Yupo wapi Sisqo Dru Hill Unleash The Dragon,Incomplete? Roxxete It must have been luv? Kci&Jojo Tell me it's real? Bow wow Puppy luv,My names is? Yupo wapi DMX Rough Ryder Anthem? Case Missing you? Massari Real luv? Wapo wapi kina Celline ambao album nzima ni hits tupu? Wapo wapi Nsync,westlife? Yupo wapi 50cent wa Get rich or die tryin? Uncle Sam I don't wanna see you again? Time will tell.
 
Hiyu P Funk alimpa makofi ya alfajiri Afande Sele nikikumbuka ile stori nacheka mpaka leo.....
 
Upo vizuri mkuu naona una library kichwani
 

Mkuu ww ni jembe...umenikumbusha kutafta hela kwa nguvu zote kipindi kabla sjazeeka....mana ukienda haurudi nyuma...khasantee mkuu
 
Ni kweli kilakitu kinamda wake, cha muhimu ni kuepuka career yako kuisha vibaya, inatakiwa unaacha legacy kiasi kwamba vizazi na vizazi vinakuwa vinaendelea kukukumbuka, kuna watu hata kama hawapo kwenye peak tena still wanaheshimika, mfano bongo watu kama Sugu, Profesa Jay, Jide, Mzee Majuto, Gurumo(r.I.p), watu kama hao wanaacha legacy kwenye career zao. Kwahiyo mabwana mdogo wakina Diamond wajitahidi kuutunza ustaa wao ili hata wakiondoka kwenye peak wasiishi maisha ya kifala
 
Nothing lasts forever, mbona kawaida tu. Mtu akiringa muacheni tu kwasababu ndio wakati wake haina haja yakumsimanga na kumuandama sana.

Hata bibi kizee aliwahi kuwa mrembo akipita watu wanageuka, teh.
 
kutesa kwa zamu
 
Master J mnamwogopa nini mleteni tumchanechane hapa awe jamvi la wenyeji hapa JF.[emoji16] [emoji16] [emoji16]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…