Kwenda chuo kuna faida ambazo form 6 hawezi kuja kuzipata, Nasisitiza kama uwezo upo nendeni chuoni, form 6 nenda ikishindikana kwenda chuo

gearbox

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2024
Posts
563
Reaction score
1,768
Special cases mtu aende form 6

Bado ni mdogo sana kiumri
Hakuna uwezo wa kumlipia ada
Kutaka kuwa mwalimu,

Background yangu, Nilimaliza form 6 miaka ya 2009 nikapiga division 2 ya 10, baada ya kufaulu ikabidi nianze kufatilia chuo, Ni kipindi ambacho wanafunzi wengi sana wanachanganyikiwa wasomee kipi, mimi binafsin nilichagua kusomea nachokipenda lakini nilipofika chuoni uhalisia ulikuwa tofauti sana na nilivyodhani, niligundua nimekurupuka kuchagua kozi, Nachoshukuru nyumbani vijihela vipo, ilibidi nibadili chuo kusoma kozi nyingine upya.

Kwenda chuo kuna faida zifuatazo

UWANJA MPANA WA KUPATA AJIRA - form 4>>chuo wana uwanja wa ajira mkubwa, wao wanaweza kuomba kazi za certificate, diploma na degree lakini wale wa form 6>>chuo wanaomba kazi za degree tu, lakini pia form 4>>chuo akipata changamoto za kushindwa kusoma degree mfano kakosa ada, anaweza kuajirika tofauti na form 6 ambae hajaweza kwenda degree hawezi kuajiriwa. form 4>>chuo na form 6>>chuo wote wanaweza kuomba ajira ya degree na wakakosa lakini form 4>>chuo anaweza kubahatika kupata kazi ya diploma au certificate, Ni kweli kazi za diploma zina mishahara midogo waweza kuta degree analipwa take home laki 8, diploma laki 5, lakini ni heri upate kitu kuliko kukosa kabisa.

Kuna kazi nyingi tu wahahitaji Diploma, Mfano nimeweka tangazo la TANROADS kuhitaji mhasibu msaidizi mwenye diploma au certificate.



ADVANTAGE YA CV - Kitu kingine ni kwamba form 4>>chuo wana cv inayovutia kiuzoefu kuzidi form 6>>chuo, ni kwamba form 4>>chuo wamesomea taaluma kwa muda mrefu zaidi darasani kuzi form 6>>chuo, wana vyeti vya kitaaluma vingi (certificate + diploma + degree) kuzidi form 6>>chuo mwenye degree pekee, na cv inaonyesha wamefanya kazi kwa vitendo maofisini (field work) mara nyingi zaidi kuliko form 6>>chuo.

URAHISI WA KUBADILI KOZI - Mtu kamaliza form 4 ana ndoto za kusomea kitu anachopenda mfano marketing, anaingia chuoni certificate mwaka moja anakuja kugudndua ni kozi anayoipenda lakini haina soko kwenye ajira, Diploma ya miaka miwili anabadili kozi kusomea labda accounting hasa ukizingatia masomo mengi walishasoma pamoja darasa moja akiwa certificate hivyo sio mgeni sana, Degree anaweza kubadilisha kozi kusomea nyingine mfano Accounting and IT ili kuongeza zaidi uwanja wa ajira za IT, Sasa tukija kwa hawa form 6>>chuo unakuta mtu anapenda kusomea insurance, anafika chuoni anakuja kugundua kitu anachokipenda kupata ajira zake ni ngumu, kubadili gia angani sio rahisi, yanabaki kuwa majuto.

KUYAZOEA MAISHA YA CHUO MAPEMA - form 4>>chuo na form 6>>chuo wote kwa pamoja wakiwa mwaka wa kwanza chuoni huwa wanapata changamoto ya uhuru wa maisha ya chuoni, style ya kusoma chuoni, kuandaa assignments, presentations, n.k. hii huwa inachangia wengi kufanya vibaya kwenye masomo mwaka wa kwanza. form 4>>chuo na form 6>>chuo wakiingia degee si ajabu kukuta Form 6 > chuo wapo wanaofaulu sana lakini muda huo huo wanaofeli zaidi na hata kudisco (kufukuzwa chuonu) ni hao hao wa Form 4.

KUYAZOEA MASOMO KWA KUYARUDIA - Na ndio sababu kubwa baadhi ya kozi za degree za miaka minne form 4>>chuo wataambiwa wasome miaka mitatu lakini form 6>>chuo watasoma minne, Ni kwamba chuoni huwa kuna kurudia rudia masomo kwenye ngazi tofauti sababu wanasomea taaluma sio vidato, kwa upande wa form 6>>chuo unakuta kasoma mambo mengi akiwa sekondari ambayo akifika chuoni hatayakuta sababu ni nje ya taaluma, atavikuta vitu vingi zaidi vipya vilivyojikita kwenye taaluma. Mfano unamkuta form 6 kasoma topics kibao za hesabu lakini wakifika chuoni wanarudia topics tatu tu na kukuta topics mpya nyingi zaidi, Muda huo form 4>>chuo kwao vitu vingi ni marudio walishavisoma sababu ni muhimu kuvijua katika taaluma, Lakini hii haimaanishi kwamba form 4>>chuo ndio wana uhakika wa kufaulu zaidi, LA HASHA !! kuna form 6 wanawakimbiza vizuri kabisa form 4>>chuo waliobweteka ama wasio na bidii.

UHURU WA KIUTU UZIMA - miaka 18+ tayari ni mtu mzima kisheria, Inashangaza kuona watu hawa wapo form 6 wana age 18+ wanatandikwa viboko, wanapangiwa mavazi, hawaruhusiwi simu, hawaruhusiwi kufuga ndevu, kusuka, n.k. ni kama watoto wadogo !! Chuoni ni tofauti uankuwa treated kama mtu mzima kisheria, hutakuja shikiwa bakora. Kuna wazazi husema wasipeleke watoto chuoni baada ya form 4 kwa kuogopa uhuru, Ukweli ni kwamba wakimaliza form 6 wataenda chuo na uhuru wataukuta, Ni suala la kuweza kuwajengea misingi watoto wajue namna ya kuishi hata wakiwa huru, hawa wanaobanwa sana ni kwaida sana wakifikaga chuoni lazima uhuru uwachanganye iwe ni form 4 ama form 6.

kwa ufupi
  • form 4>>chuo kasomea miaka mingi zaidi taaluma kuzidi form 6>>chuo
  • form 4>>chuo kafanya mazoezi ya kazi kwa vitendo mara nyingi zaidi kuzidi form 6>>chuo
  • form 4>>chuo ana vyeti vingi vya taaluma (certificate+diploma+degree)
  • form 4>>chuo badhi ya vyuo akiingia degree anasomea miaka mitatu tu, yule wa form 6>>chuo ni mgeni sana inabidi asomee miaka minne
  • form 4>>chuo anatambulika kitaaluma akihitimu diploma, cheti cha form 6 hakitambuliki kwa taaluma yoyote
  • ikitokea mzazi kaishiwa pesa, hakuna mkopo wa chuo, n.k. kwenda kusoma degree, form 4>>chuo anaweza kuajiriwa bila degree, form 6 hawezi kuajiriwa hata kama ana division 1.
 
Form six ni mihimu kujenga maturity na reasoning capacity ya mtoto, sio kila mtu anasoma kuajiriwa, vyuo vya kati au vya diploma na basic certificate vibaki kua vya watoto kutoka kaaya masikini.
 
Umetisha kwa upembuzi yakinifu mkuu, lakini wachache sana watakuelewa
 
Hakuna point hapo mkuu ni ujinga mtupu.
Kaangalie ajira zinazotangazwa uone idadi nyingi zinahitaji diploma au bachelor. Labda kama ndoto zako kupiga upolisi
 
Mkuu umechambua vema sana hujaacha kitu.

Vyuoni waliopita form 4>>certificate >>diploma ni moto wa kuotea mbali wanawaacha mbali sana form 6 fresh from school.

Watoto wangu kamwe sitaruhusu wakapoteze muda form 6 isiyo na tija yoyote maana mtu anamaliza form 6 hana taaluma yoyote lakini mwenzake aliyepita diploma tayari ana taaluma.
 
Hakuna point hapo mkuu ni ujinga mtupu.
Kaangalie ajira zinazotangazwa uone idadi nyingi zinahitaji diploma au bachelor. Labda kama ndoto zako kupiga upolisi
Nafasi za diploma zipo nyingi sana kuanzia serikali kuu hadi serikali za mtaa.

Tena kwenye afya nafasi za diploma ndiyo za kumwaga.
 
Kusoma chuo siyo kwa ajili ya kutafuta ajira, lengo kuu ni kupanua upeo wa kuona mambo mbalimbali na kuimarisha uwezo wa kutafsiri mambo unayoona. Unaweza kujisomea nyumbani na kujipatia elimu hiyo, lakini muundo wa chuo huwa ni mzuri na wenye ufanisi sana katika kutoa elimu kwa njia ya haraka kuliko kujisomea mwenyewe nyumbani.

Kwa mfano kuelewa tu kuwa kwa nini himaya ya kirumi ilianguka, inakusaidia pia kujua kuwa wewe kama binadamu katika maisha yako ya kila siku iwapo utajiweka katika nafasi ya himaya ya kirumi na kuendesha maisha yako kwa mtindo wa wataalamu wa Kırım’ı utaanguka.
 
Mtu wa form6 huwezi linganisha na mtu wa diploma. Kama unajiweza kielimu na una kichwa chepesi kasome form6 ila kama uliibia form4 au hujiwezi sana kielimu basi nenda diploma.

NB1: bado nakumbuka watu wa diploma walivyoliwa kichwa mwaka wa kwanza.. hii inaonesha kiasi gani mtu wa form6 alivyo smart kichwani kielimu.

NB2: kama una nia ya kusoma MD badae usijiloge ukaenda kusoma diploma.
 
mkuu je wewe ulisoma advance level
 
Form six ni mihimu kujenga maturity na reasoning capacity ya mtoto, sio kila mtu anasoma kuajiriwa, vyuo vibaki kwa watoto kutako kaya masikini
Mimi nimesoma form 6 kawadanganye wengine

hebu tueleze form 6 inajenga vipi maturity wakati wanafunzi wanachukuliwa kama watoto wadogo wanatandikwa bakora kisa wamechelewa kuhesabiwa, wanapewa adhabu kisa hawajavaa tai, wanapangiwa muda wa kulala, hawaruhusiwi kumiliki simu za mawasiliano, n.k.

Chuo ndio kinamjenga mtu zaidi maturity na reasong capacity,

  • kujifunza kupangilia bajeti ya pesa za matumizi kila mwezi
  • kujifunza kuweka mipaka kwenye uhuru
  • Kujinza kuwa accountable kwenye maamuzi yao ya maisha huru
  • Time management kubalance muda wa masomo na maisha binafsi yenye uhuru
  • kujifunza kufanya kazi maofisini na teamwork.
  • kufanya reseach
  • n.k.
 
Hakuna point hapo mkuu ni ujinga mtupu.
Kaangalie ajira zinazotangazwa uone idadi nyingi zinahitaji diploma au bachelor. Labda kama ndoto zako kupiga upolisi
unaongea kwa hasira bila takwimu, kazi kibao za assistant zinahitaji diploma
 
Sikuhizi wanafunzi na wazazi wameamka wamekuwa wajanja, form 4 wenye division 1 na 2 wapo vyuoni wamaeona ujanja ni kusomea taaluma zao mapema, Kuanza kusomea career zao mapema, mambo ya form 6 yalikuwa kipindi cha zamani enzi hizo hata darasa la saba anaajiriwa serikalini.
 
Huwezi linganisha degree holder aliyepitia form6 na wa diploma! Hawa ni watu wawili tofauti.

Injinia aliyepitia form6 ana uwezo mkubwa (hasa katika sanifu) kuliko aliyetoka diploma.
 
mkuu je wewe ulisoma advance level
Nilisoma Form 6 kwasababu kwa enzi zetu mwamko wa kwenda chuoni ulikuwa ni mdogo sana, tulikuwa tunadanganywa kwamba kwenda chuo ni kwa wale wanaopata D nne form 4 kumbe hata division 1 unaenda fresh tu, muda ungerudi ningeenda chuo !!
 
Huwezi linganisha degree holder aliyepitia form6 na wa diploma! Hawa ni watu wawili tofauti.

Injinia aliyepitia form6 ana uwezo mkubwa (hasa katika sanifu) kuliko aliyetoka diploma.
Acha kujidanganya, vuta stuli nikupe uhalisia

  • Injinia wa form 4>>chuo kasomea miaka mingi zaidi taaluma kuzidi form 6>>chuo
  • Injinia wa form 4>>chuo kafanya mazoezi ya kazi kwa vitendo mara nyingi zaidi kuzidi form 6>>chuo
  • Injinia wa form 4>>chuo ana vyeti vingi vya taaluma kuzidi form 6>>chuo aliyechelewa kuanza kusomea taalum
  • injinia wa form 4>>chuo akiingia degree anasomea miaka mitatu tu, yule wa form 6>>chuo ni mgeni inabidi asomee miaka minne
  • injinia wa form 4>>chuo anatambulika kitaaluma ni engineer akihitimu diploma, Kwa form 6 hata uwe na divisioni 1 ya PCM, PGM, n.k. hutambuliki wa taaluma yoyote wala huwezi kuajiriwa
 
1. Siwezi jidanganya naongelea uzoefu. Chuoni diploma walio graduate hawakuzidi watatu. Bado unataka niambia diploma wako vizuri kuliko form6?

2. Kuhusu mazoezi huwezi niambia mtu wa diploma kafanya mazoezi mda mrefu kuliko injinia anayepitia form6. Je unajua chuoni kuna field ya miaka 3?

3. Kuhusu diploma kusoma miaka 3 sio always the case. Chuo kikuu (nasema the like of udsm, sua, aru nk nk) haijalishi umesoma diploma au 6 wote lazima msome miaka minne. Naongelea uzoefu nilioona.

Narudia tena huwezi linganisha injinia wa form6 na injinia wa diploma. Form6 ni ishara ya mtu anayejiweza kielimu.
 
Usiangalie idadi, kigezo ni kwamba hao form 4>>chuo mme graduate wote na hampo sawa, yeye kaanza kusoma chuo baada ya form 4, mpo tofauti, na ndicho post hii inahusu.

Tumia common sense, Mtu aliesomea diploma mkakutana degree lazima awe kapitia mazoezi mengi ya kikazi, Mazoezi ya degree mtayofanya wote ukijumlisha na mazoezi yake ya diploma, automatically anakuwa na idadi kubwa ya mazoezi kikazi

Ok, hata kama kuna vyuo form 4>>chuo na form 6>>chuo wote wanasoma miaka minne degree ni sawa tu, anaongeza vyeti zaidi, anaongeza experience zaidi ya kufanya kazi kwa vitendo, anaongeza miaka ya kusomea taaluma zaidi,

Pia form 4>>chuo anapomaliza diploma tayari anatambulika kwa taaluma ni engineer na anaweza kuajiriwa, kwa upande wa form 6 hata awe na division 1 ya PCM, PGM, n.k. hatambuliki kwa taaluma yoyote. ikitokea wote wameshindwa kwenda degree, form 4>>chuo ana nafuu in terms of career.

cant be the same, just get over it !!
 
Tufunge mjadala:
Tuache watoto wachague pale wanapopenda. Miruzi mingi hupoteza mbwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…