Elections 2010 Kwenu ameahidi nini?

Malila

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2007
Posts
5,329
Reaction score
5,024
Kwa kweli mgombea wa CCM anachemsha vibaya, 2005 kwetu alituahidi umeme toka Makambako mpaka Songea mjini. Hamna cha umeme wala nini? Juzi CCM wameahidi kujenga reli toka Mtwara mpaka Songea ndani ya miaka mitano ijayo, wa kumuuliza hatumwoni,mbunge wetu kahamia Dsm. Ipo haja kukusanya ahadi zote alizotoa ili watu wake wamkumbushe kwamba mzee punguza.

kwenu kaahidi nini?
 
kUNA JAMAA ALISHAANZISHA THREAD YA AHADI ZA HUYU JAMAA...NI NYINGI AJABU, NA HAWEZI KUZITEKELEZA HATA ROBO HADI MWISHO WA MAISHA YAKE!
Anawajua Watz ni mabingwa wa kusahau!
 
Inauma sana/inatisha sana lakini ipo siku moja chini ya jua hili hili mambo yanabadilika. Dalili si mbaya.
 
Ameahidi barabara za juu, wakati za chini hakuna.

mix with yours!!
 
Ameahidi viwanja vipya vya ndege vya kimataifa wakati ndege hakuna, wameua atc
 
Ameahidi ambulance za bajaji vijiji wakati hakuna barabara
 
 
Kwetu kuna matatizo ya maji na ametuahidi atatuleta bahari.
 
Mbulu, katuahidi maji tele, hospital ya Haydom Lutheran kuwa ya rufaa.
 
Kwetu alikuja akaahidi daraja la kisasa tuweze kuvuka mto kirahisi . Tukamwambia hatuna mto. Akaahidi kutuletea na mto pia.
 
kwetu kaahidi kununua mashamba yote ya maswahiba wake atugawie wadanganyika bila kusahau vyandarua feki vya Bush!!!
 
Ameahidi kubadili kijiji chetu ili yawe makao makuu ya umoja wa mataifa!
 
jimboni kwetu tunashindia mlo mmoja. mkewe ametushauri tule keki zinafaa kwa kipindi hiki kigumu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…