mluga
JF-Expert Member
- Oct 8, 2010
- 676
- 215
Bunge la katiba, limeanza kukaa kujadili kile ambacho watanzania wengi wanakisubiri kuwezaa kujua hatima ya nchi yetu. Wabunge wa bunge hili wabemba au wamebebeshwa kazi kubwa saana, ambayo busara na hekima yao inaweza kuiingiza nchi hii katika vita au kuiweka katika nuru iliyojaa upendo na amani. Kwa nini nimetumia kichwa hiki cha habari chenye swali au kukumbushana nini tumejifunza kutoka nchi hizo, ingawa mauaji katika nchi hizo, kuna mtu anaweza kushindwa kuelewa inashabihiana vipi na uandishi wa katiba yetu? Hilo baada nitalionyesha.
Ndugu, wapendwa watanzania wenzangu, sote tumeshuhudia kazi kubwa iliyofanywa na tume ya warioba, kukusanya mawazo na nini watu wanafikiria na kukitaka kwa ustawi wa nchi yao. Tumeshuhudi mihadhara ya kundi la UAMSHO kuhusu kuitaka Zanzibar ilo na mamlaka kamili. Hata kama kundi hili halikuwa na ruhusa, lakini kwa misingi ya utawala bora na wa kidemokrasia lazima tuheshimu mawazo ya watu. Huwezi kuzima mawazo ya watu wengi kwa nguvu.
Takwimu zilizokusanywa na tume ya Warioba, na ukiangalia hiyo mihadhara hakuna unapoweza kuficha ukweli kuwa Zanzibar inataka mamlaka kamili.
Mwaka 2010, kama sijakosea Zanzibar ilifanya mabadiliko makubwa saana katika katiba yake ambayo ilimyima kabisa hadhi na mamlaka Raisi wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Sasa cha kujiuliza hivi wajumbe wa kamati kuu ya CCM Zanzibar walikuwa wapi? kulikemea hilo na kwa nini kama kweli wanataka muungano wa serikali mbili walikaa kimia?
Mbona waliweza kumthibiti Karume asibadilishe kipengele cha ukomo wa kuwa raisi?
Usalama na utulivu wa Zanzibar kuelekea swala la mamlaka kamili, ukiuutazama kwa undani ni watu wawili tu ndo wameshikiria , nao ni makamu wa kwanza wa Raisi na katibu mkuu wa CUF maalim Seif Sharif Hamadi na Raisi Mstaafu wa Zanzibar Amani Abeid Karume.
Tumeshuhudia machafuko ya chini chini kuwalenga watu wenye asili ya Tanzania bara, hata kuuawa, sasa tujiulize kwa population ya Zanzibar, na mila na desturi za visiwa hivi ambavyo watu wake wameingiliana saana. Je inawezekana mpaka leo kweli hawa wanaofanya, au kundi linalofanya mambo haya lisijulikane?
Muungano ni wa watu, na wala hakuna sababu ya kutumia mabavu kulazimishana. Swala hili ni nyeti saana kuliko walio wengi tunavyolichukulia kuwa upepo utapita. ukitazama midahalo ya watu hawa, ni kuwa watu wako tayari kwa lolote ni kuwa wanachosubiri ni baraka za uongozi wao.
Athari ambayo nataka WABUNGE muikukumbuke, na histori itakuja kuwakumbusha ni kuwa leo hii watu wa Zanzibar wakicharuka na kuanza kuwaua watu wa Bara, na baadae watu wa bara waje kuanza kulipiza kisasi kwa yeyote anatoka zanzibar, tusije shangaa kujikuta Tanzania yanatukuta kama haya yaliyotokea CAR.
Wabunge tumieni busara, na kuweka pembeni mambo ya vyama, usalama na umoja wa Tanzania unategemea busara na utu wenu.
kuna umuhimu mkubwa wananchi wa Zanzibar, waheshjimiwe matakwa yao, hakuna haja ya kulazimisha, tutaiua nchi yetu huku tunaiona. Angalieni KIEV, Ukraine, inavyowaka moto leo, kwa tamaa za wachache.
Tulishuhudia Ivory Coast, ikiharibika kwa tamaa za wachache.
Mungu Ibariki Tanzania