Juzi nikua mkoani Mbeya na Tunduma katika safari zangu ila kwa nilichoshuhudia ni mateso sana, sijui tatizo nini. Sikuweza kupata usafiri wa saa 12 alfajiri kwahiyo nikaja Uyole kuvizia usafiri wowote. Jamani, tulipandishwa bus aina ya fuso ambalo lilituacha Makambako!
Mpaka tunafika Dar tulikuwa tumepanda bus 4, kisa hizo gari 'za hakuna' kulala haziruhusiwi, na abiria ni wengi kupita maelezo. Hizi gari zilikuwa zinasaidia sana pale Uyole maana wasafiri kutoka Malawi, Zambia wanaochelewa asubuhi tunapanda nao, kuzikataza imekua ni kero kubwa sana, sijui mbadala wake ni upi.
Mama anafungua nchi, RC anasema K/Koo iwe 24/7 wageni waje na kufanya biashara, sasa wanakwama hapo Uyole, usafiri ni shida. Ruhusuni bus kubwa muwape ratiba ya mchana au hizo coaster muwape vibali wafanye biashara, hali ni mbaya sana, nadhani wakazi wa Mbeya mtakua mnaelewa.