Kwenu ma doctor wa mifugo/wanyama

Kwenu ma doctor wa mifugo/wanyama

wa stendi

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2016
Posts
25,190
Reaction score
27,434
Katika wanyama upande wa ng'ombe kuna siku tulichinja ng'ombe na baada ya kumchuna ngozi tulimpasua na kumkatakata kugawa nyama, lakini la kushangaza kwenye nyama yake mle ndani ya steki maeneo ya mbavuni juu karibu na bega la mguu wa mbele tulikuta kitu kama uvimbe chenye ukubwa kama ile mpira wa watoto 'tenesi' ndani ya kile kitu baada ya kukipasua japo kilikuwa ni kigumu na ndani tumekuta manyoya na vitu kama vyeusi vyeusi kama damu iloganda na vimawe mawe kama firigisi fulani,hivi huwa ni kitu gani kile na je kwenye mwili wa mnyama huwa kina madhara huko mbeleni kama tusingechinja yule ng'ombe je angekufa au hii ni hali ya kawaida kwa kila mnyama kuwa na kitu kama hicho katika mwili.

Naomba kujuzwa.
 
Baba yangu aliniambia kuwa kitu hicho ni kinga yake aliowekewa na Mungu, alisema kuwa kidude hicho kina manyoya ya wanyama wote wanaopatikana duniani,alisema kuwa ng'ombe wa aina hiyo akiwa katikati ya kundi la wenzake au akiwe peke yake eneo hilo simba hagusi na kinapatikana kwa ng'ombe wachache sana.
 
Huwenda ni kweli maana nina uzoefu sana wa kuhudhuria machinjioni ila nimeona kama mara mbili tuu kwa uzoefu wangu ..
Vipi hajakuambia kinaitwa nini

Aliniambia kwa kiluga kuwa inaitwa nchilizi, kwa kiswahili hirizi.
 
Katika wanyama upande wa ng'ombe kuna siku tulichinja ng'ombe na baada ya kumchuna ngozi tulimpasua na kumkatakata kugawa nyama, lakini la kushangaza kwenye nyama yake mle ndani ya steki maeneo ya mbavuni juu karibu na bega la mguu wa mbele tulikuta kitu kama uvimbe chenye ukubwa kama ile mpira wa watoto 'tenesi' ndani ya kile kitu baada ya kukipasua japo kilikuwa ni kigumu na ndani tumekuta manyoya na vitu kama vyeusi vyeusi kama damu iloganda na vimawe mawe kama firigisi fulani,hivi huwa ni kitu gani kile na je kwenye mwili wa mnyama huwa kina madhara huko mbeleni kama tusingechinja yule ng'ombe je angekufa au hii ni hali ya kawaida kwa kila mnyama kuwa na kitu kama hicho katika mwili.

Naomba kujuzwa.
Kitaalam inaitwa lymph node
 
Back
Top Bottom