wa stendi
JF-Expert Member
- Jul 7, 2016
- 25,190
- 27,434
Katika wanyama upande wa ng'ombe kuna siku tulichinja ng'ombe na baada ya kumchuna ngozi tulimpasua na kumkatakata kugawa nyama, lakini la kushangaza kwenye nyama yake mle ndani ya steki maeneo ya mbavuni juu karibu na bega la mguu wa mbele tulikuta kitu kama uvimbe chenye ukubwa kama ile mpira wa watoto 'tenesi' ndani ya kile kitu baada ya kukipasua japo kilikuwa ni kigumu na ndani tumekuta manyoya na vitu kama vyeusi vyeusi kama damu iloganda na vimawe mawe kama firigisi fulani,hivi huwa ni kitu gani kile na je kwenye mwili wa mnyama huwa kina madhara huko mbeleni kama tusingechinja yule ng'ombe je angekufa au hii ni hali ya kawaida kwa kila mnyama kuwa na kitu kama hicho katika mwili.
Naomba kujuzwa.
Naomba kujuzwa.