Kwenu mnaolalamika kuwa wasichana wanapenda pesa

Kwenu mnaolalamika kuwa wasichana wanapenda pesa

Fauya

JF-Expert Member
Joined
Sep 19, 2017
Posts
262
Reaction score
479
Nyie mnaolalamika wanawake wa sikuhizi wanapenda hela inaonesha hamjakaa na bibi zenu wakawaambia maisha yalivokuwa kipindi hicho miaka ya 1940, 50, na miaka ya zamani mingine.

Mwanamke alikua anaolewa na mwanaume mwenye uwezo wa kumuhudumia yeye pamoja na watoto wake na pia ikitokea tatizo ukweni mwanaume awe na uwezo wa kulitatua. Biblia inasema tuishi na wake zetu kwa akili, lakini umewahi kujiuliza ni akili ipi inayoongelewa hapo?

Huku mjini kulingana na mabadiliko ya teknolojia na utandawazi mtu mwenye akili ni yule mwenye gari mwenye nyumba mwenye uwezo wa kubadili mboga mwenye uwezo wa kuvaa na kupendeza mwenye uwezo wa kumiliki simu kali yaani kiufupi mtu mwenye pesa ndo ana akili kwa mantiki hiyo wanawake wanavotaka kuwa na mwanaume mwenye pesa ni wanatimiza neno la Biblia na pia ni asili ya mwanamke kuwa na mwanaume mwenye uwezo wa kumhudumia.

Marehemu bibi yangu aliwahi kunambia kipindi akiwa msichana mdogo wapo wanaume wengi waliokua wanataka wamtolee mahari lakini alimchagua babu kwasababu alikua anafanya kazi na anapata pesa (babu yangu alikua capenter)
 
Ukikua utaacha ujinga, na utajiunga kwenye Chama cha Wanaume Bahiri Tanzania (UWABATA), ngoja tukupe muda.

KATAA NDOA, KATAA MATAPELI.

KaziKweliKweli/JobTrueTrue
Lengo la kuwa bahili ni ili usitumie pesa na hutaki kutumia pesa kwakua hauna, ila ukizipata utaacha ubahili
 
Mwanamke alikua anaolewa na mwanaume mwenye uwezo wa kumuhudumia yeye pamoja na watoto wake na pia ikitokea tatizo ukweni mwanaume awe na uwezo wa kulitatua.
Hilo suala waliifunga Safari wakasafiri mpaka Beijing 1995 -Fourth World Conference on women beijing 1995 kwenda kulivunja kwa pamoja na wakalitungia Sheria na sasa hivi wamekuja na ajenda mpya Mwanamke hakuna kutegemea kitonga Ganda la ndizi hata wale vitimaalum Bungeni waliochomekwa tu bila kupigiwa kura wamesema wanataka wachomolewe, sasa unataka kusemaje waendelee kufanya wakati kuna wenzao tangu 1995 wanapiga Vita udangaji?
 
Kuna tofauti kati ya udangaji na kuolewa. Wale wanaodanga wajihudumie wenyewe ila wale walioolewa wahudumiwe na waume zao.
Shida inakuja pale mdangaji anapoolewa
 
Kwakulijua hilo ndiyo maana nasisi tunatafuta wasichana wenye ajira zao hapa mujini ili kubalance mizani Wengine wanaenda mbali wanaona bora kulelewa ili kukwepa kuelemewa na uzito wa majukumu
 
Back
Top Bottom