4 7mbatizaji
JF-Expert Member
- Dec 8, 2019
- 8,406
- 9,619
Ndugu zangu nawasalim wote wakubwa kwa wadogo kupitia yule atupae pumzi.
Kichwa cha habari hapo juu chahusika na tukiwa tumebaki na siku mbili kuwapigia viongozi wetu tuwatakao, hivyo zingatia yafuatayo
1. Tafadhali sana kapige Kura, na chagua kiongozi umpendaye bila shurti ya mtu yeyote
2. Tuna wagombea wengi ila kwa kweli CHADEMA na CCM ndo habari ya mjini na Moto unawaka kwa vyama hivi viwili, mtoto hatumwi sokoni na hivyo kwenye karatasi ya wagombea urais CCM chini ya mgombea wao yupo namba moja na CHADEMA chini ya mgombea wao a.k.a Simba wa Yuda, kimbunga Lissu 2020, au wengine husema mbeba maono, ni wa mwisho, namanisha ndo amefunga karatasi ya wapiga Kura.
3. Upigapo Kura punguza hasira au furaha moyoni mwako ili usiharibu Kura ya mgombea unaemtaka. Weka vema kwenye kisanduku cha mgombea umpendae isitoke nje ya kibox na usifanye cha ziada mfano Kama kutoboa macho ya mgombea utakuwa umeharibu Kura.
4. Kura ni Mali yako maana we ndo mwajiri wa viongozi wako kuanzia diwani, mbunge, mpaka rais hivyo una haki kulinda Kura yako au kutoilinda Kama Kuna mtu unaemwamini atakulindia kura yako kwa niaba yako
Mwisho ndugu zangu: Mungu awasimamie katika kutimiza wajibu huu muhimu ili kuwaajiri viongozi wema. Barikiwa Sana kwa ujumbe huu