Balantanda
JF-Expert Member
- Jul 13, 2008
- 12,480
- 4,775
Hivi TFF kwa nini hawabadiliki?,wataachana lini na tabia hii ya kuahirishaahirisha mechi za ligi kuu ya VodaCom na kuvuruga ratiba?,soma habari hii hapa chini toka gazeti la MwanaSpoti,inakera...
AIBU YA MWAKA
FRANK SANGA
KWA neno jepesi unaweza kusema ni aibu. Lakini kukosa mipango, ubabaishaji na kuendesha mambo kienyeji kumedhihirika tena katika soka ya Tanzania.
Kama televisheni ya Skysport ambayo ina haki ya kuonyesha Ligi Kuu England ingekuwa na mkataba wa kuonyesha mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara, kesho Jumapili wangevunja mkataba huo.
Skyports ina mkataba wa kuonyesha laivu mechi 92 za Ligi Kuu England huku ESPN ya Marekani ikipewa haki ya mechi 46. Na hakuna shaka kama wangekuwa wanaonyesha mechi za Ligi Kuu Tanzania kesho Jumapili ingekuwa ndio mwisho wao.
Hata wadhamini wa Ligi Kuu Bara, Vodacom wakiamua kujitoa hakuna ambaye atawalaumu kutokana na ubabaishaji ulionyeshwa jana Ijumaa katika medani ya soka Tanzania.
Mechi ya watani wa jadi, Simba na Yanga ambayo imetangazwa kwa zaidi ya miezi saba kuwa ingefanyika kesho Jumapili, imeahirishwa ghafla na sasa itafanyika Jumapili ya Aprili 18 huku baadhi ya mashabiki wakiwa wamesafiri kuja Dar es Salaam kutoka mikoa mbalimbali.
Kwa mara nyingine, Serikali imedhihirisha haijifunzi na kurudia makosa yake ya miaka ya nyuma baada ya waziri aliyekuwa na dhamana ya kusimamia michezo wakati huo, Profesa Juma Kapuya alipolazimisha timu nane kushiriki ligi ya "Nane Bora' wakati makubaliano na wadhamini yalikuwa ni timu sita 'Sita Bora'.
Ni miaka hiyo ya mwishoni mwa tisini wakati misimu miwili timu hazikushuka daraja kutokana na msimamo wa waziri huyo.
Hatua hiyo ilisababisha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kujiondoa kudhamini ligi hiyo kutokana na kuona hatua hiyo ilikuwa kinyume cha makubaliano yao na kilichokuwa Chama cha Soka Tanzania (FAT).
Mmoja wa wachambuzi wa soka nchini aliliambia Mwanaspoti kuwa hiyo ni aibu kubwa na inaweza kuathiri matangazo ya televisheni, redio, wadhamini na kupunguza mashabiki wa soka.
"Kama Supersport wangetoka Afrika Kusini kuja kuonyesha mechi hii, ingewaje iwapo wangefika na vifaa vyao na kuambiwa mechi imeahirishwa? " Alihoji mchambuzi huyo maarufu wa soka.
"Makampuni yanafanya biashara, hayataki kujihusisha na ubabaishaji, hivyo iwapo wadhamini wakijitoa hakuna wa kulaumu, kwani huu ni ubabaishaji," alisema.
Habari kutoka ndani ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), zinadai kuwa serikali imetoa shinikizo kuahirishwa kwa mechi hiyo ikitaka ifanyike kwenye Uwanja wa Taifa, licha ya kujua kuwa Simba na Yanga zilitangaza tangu mwanzoni mwa wiki kuwa wangefanyia mechi hiyo Uwanja wa Uhuru kukwepa gharama kubwa Uwanja wa Taifa.
Kuahirishwa kwa mechi mara nyingi hutokana na sababu za msingi na zisizokwepeka mathalani maji kujaa uwanjani, barafu au majanga mbalimbali.
Kutokana na hilo, kocha wa Yanga, Kosta Papic amegeuka mbogo baada ya kuambiwa mechi yao dhidi ya Simba imeahirishwa na ameiita kuwa ni hujuma, lakini Kocha wa Simba, Patrick Phiri akasema: "Ndio maisha haya."
Papic na Phiri walizungumza na Mwanaspoti jana Ijumaa kwa muda tofauti kuhusu kuahirishwa kwa mechi hiyo.
Papic kutoka Serbia aliiambia Mwanaspoti kuwa, kitendo hicho ni aibu kubwa na kinatia hasira kwani si uamuzi sahihi kuahirisha mechi kubwa kama hiyo.
"Nina hasira, tumefanya maandalizi siku zote kwa wiki nzima, halafu watu wengine wanakutana na kuahirisha mechi," alilalamika kocha huyo aliyezaliwa mwaka 1960.
Papic maarufu kwa jina la Bill Clinton alisema aliandaa timu yake vizuri na wachezaji wake walikuwa katika morali ya juu, hivyo kitendo hicho kimewakatisha tamaa kwani ni muda mrefu Yanga haijacheza mechi ya mashindano.
"Tumekaa muda mrefu bila kucheza mechi, hii inaweza kutuathiri. Tumejiandaa vizuri, wachezaji na mimi, wote tuna hasira sana kwa uamuzi huu, hatuelewi tufanye nini. Gharama hizi nani atalipa hotelini? " Alihoji Papic mwenye watoto wawili kwa mke wake, Milka.
Papic ambaye alikuwa anazungumza kwa hasira alisema haelewi kama awarudishe nyumbani wachezaji wake au aendelee kuwaweka katika kambi iliyopo kwenye Hoteli ya Holiday Inn, Dar es Salaam.
Lakini Phiri alizungumza kwa hadhari na ufupi na kusema kuwa suala hilo ni la kiutawala, hivyo hawana jinsi ya kufanya.
"Hatuwezi kufanya lolote, ndio tayari imetokea, tunachotakiwa ni kukaa chini na kujipanga upya, ingawa tulikuwa tumemaliza mandalizi yetu," alisema kocha huyo wa Zambia.
Phiri aliyezaliwa mwaka 1956 alisema katika maisha ya binadamu kuna mambo mengi yanayotokea kila mara na hii ni sehemu ya maisha hayo.
"Ndio maisha," alisema Phiri: "Tulijiandaa kwa mechi ya Jumapili, lakini kila kitu kimebadilishwa kwa hiyo tunatakiwa kujiandaa kwa mechi ya Aprili 18, hatuna jinsi," alisema Phiri kutoka Zanziba