Kwenu walevi wenzangu

certified mdokozi

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2016
Posts
1,403
Reaction score
814
Natumain sisi sote ni wazima na tupo juu ya viti virefu tukihakikisha watoto wanapata elimu iliyo bora, barabara zikijengwa kwa viwango na dada, wake na mama zetu wanapoenda hospitali wanapata huduma nzuri, na wale wadogo zetu wanapata fedha zao za kujikimu huko hospitalini achiliaa wale wenye dharau majigambo na majivuno tukienda maofisini mwao ambao kadri unavyoshusha kiraji unaweka % kadhaa kwenye mshahara wake.

Hivi sasa wale wa UKUTA wanatusubiri maana sisi pekee ndo majemedari wazuri wa vita tukisha twika viroba hakuna wa kusimama mbele ya msafara zaidi yetu hvyo mabomu vilungu na maji ya washawasha yote huwa yanaanza kwetu.

Niwasihi tu ndugu zangu jukumu la kuijenga hii nchi mara zote limekuwa letu kwa asilimia 75% maana sisi ndo hatulalamiki kadri wanavyopandisha bei za vilaji vyetu afya yetu ni muhimu sana kwa gurudumu la maendeleo la hili taifa.

Hawa mbaya zaidi hawatujui tunaitwa WALALAHOI majukwaani , Tunaitwa WAZEMBE NA WAZULULAJI kila tukikutwa bar asubuhi au usiku tukiwa tunarudi kujilaza vibandan mwetu maofisin mwao wanatuita WAMACHINGA, WAKULIMA kifupi si watawala wala hawa tunaoenda kuwajengea UKUTA wanao thamini mchango wetu alaf cha ajabu wengi ni miongoni MWETU sisi.

Niwasihi tu sisi Tukae pembeni kidogo na hii vita maana vita vingi vya namna hii huwa mwishon vinafaida na makundi baadhi ila si hili letu na bado sisi ndo Tutakuwa wajenga nchi wachumi wote wa nchi hii walifundishwa kodi ipo KWETU watawala wote wa nchi hii walifundishwa kutusakama sisi, mwisho nipende tu kuwasisitiza popote ulipo kama unacho usiache kumpa mwenzio kaofa hata ka mbili moto (usimpe baridi atakosa moyo wa kutafuta ya pesa za kununua zake ) maana huu uchumi wote mnauona ngoja mm nimalize hili fundo niwah home[emoji481]
 
Duuh!Mimi mida yangu bado..!mwenzangu tangulieni tuuh bar..nyama choma muimu.
 
Kata kileo ujinga ukutoke ngoja nami mikate lock maana nilikuwa sina ratiba hiyo asante kwa kunikumbusha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…